Date: 
03-12-2022
Reading: 
Mathayo 3:1-4

Hii ni Advent 

Jumamosi asubuhi tarehe 03.12.2022

Mathayo 3:1-4

[1]Siku zile aliondokea Yohana Mbatizaji akihubiri katika nyika ya Uyahudi, na kusema,

[2]Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

[3]Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, 

Sauti ya mtu aliaye nyikani, 

Itengenezeni njia ya Bwana, 

Yanyosheni mapito yake.

[4]Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwitu.

Bwana anakuja tuandae mioyo yetu;

Yohana Mbatizaji alimtangulia Yesu akihubiri juu ya ujio wa Mwokozi wa ulimwengu, Yesu Kristo. Aliwaambia watu kuandaa mioyo yao kumpokea Mwokozi ajaye, maana ni mkuu sana, ambaye Yohana alisema hakuwa na uwezo wa hata kufungua viatu vyake.

Yohana aliwaambia watu kutubu dhambi kwa maana ufalme wa mbingu umekaribia. Aliwataka kutubu dhambi kumpokea Kristo.

Toba ni muhimu sana kwa kila aaminiye, ndiyo maana Yesu Kristo alihimiza toba mwanzoni kabisa mwa kazi yake;

Mathayo 4:17

[17]Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.

Tunajiandaa kukumbuka Yesu alivyozaliwa duniani, lakini pia jinsi atakavyorudi kwa mara ya pili kulichukua Kanisa ambapo watakaoingia mbinguni ni wale waliomwamini, wakampokea na kumfuata. Tuhakikishe kabla hatujalala tumesamehewa dhambi zetu, maana Bwana anakuja tuandae mioyo yetu. 

Nakutakia Jumamosi njema.