Date: 
17-11-2021
Reading: 
Mathayo 25:14-30 (Matthew)

JUMATANO TAREHE 17 NOVEMBA 2021, ASUBUHI

Mathayo 25:14-30

14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.
17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.
18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.
19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.
20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.
21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.
23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.
26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
28 Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.

Hukumu ya mwisho;

Yesu alitoa mfano wa talanta, ambapo wawili walikuwa waaminifu katika mali waliyopewa, wakazalisha, na bwana wao akawaweka juu ya mengi.

Tunaitwa kutumia vipawa tulivyopewa kwa ajili ya Bwana, maana kazi ya Mungu inatuhusu. Uvivu haufai, maana hudumaza kazi ya Mungu.

Tafsiri pana ni kuwa watendakazi waaminifu wa Mungu ili neema yake isitupungukie, na siku akirudi tuingie uzimani. Siku njema.


WEDNESDAY 17TH NOVEMBER 2021, MORNING

Matthew 25:14-30

The Parable of the Talents

14 “For it will be like a man going on a journey, who called his servants[a] and entrusted to them his property. 15 To one he gave five talents,[b] to another two, to another one, to each according to his ability. Then he went away. 16 He who had received the five talents went at once and traded with them, and he made five talents more. 17 So also he who had the two talents made two talents more. 18 But he who had received the one talent went and dug in the ground and hid his master's money. 19 Now after a long time the master of those servants came and settled accounts with them. 20 And he who had received the five talents came forward, bringing five talents more, saying, ‘Master, you delivered to me five talents; here, I have made five talents more.’ 21 His master said to him, ‘Well done, good and faithful servant.[c] You have been faithful over a little; I will set you over much. Enter into the joy of your master.’ 22 And he also who had the two talents came forward, saying, ‘Master, you delivered to me two talents; here, I have made two talents more.’ 23 His master said to him, ‘Well done, good and faithful servant. You have been faithful over a little; I will set you over much. Enter into the joy of your master.’ 24 He also who had received the one talent came forward, saying, ‘Master, I knew you to be a hard man, reaping where you did not sow, and gathering where you scattered no seed, 25 so I was afraid, and I went and hid your talent in the ground. Here, you have what is yours.’ 26 But his master answered him, ‘You wicked and slothful servant! You knew that I reap where I have not sown and gather where I scattered no seed? 27 Then you ought to have invested my money with the bankers, and at my coming I should have received what was my own with interest. 28 So take the talent from him and give it to him who has the ten talents. 29 For to everyone who has will more be given, and he will have an abundance. But from the one who has not, even what he has will be taken away. 30 And cast the worthless servant into the outer darkness. In that place there will be weeping and gnashing of teeth.’

Read full chapter

Footnotes

  1. Matthew 25:14 Or bondservants; also verse 19
  2. Matthew 25:15 A talent was a monetary unit worth about twenty years' wages for a laborer
  3. Matthew 25:21 Or bondservant; also verses 232630

 

Final Judgment;

Jesus gave the parable of the talents, in which two of the given were faithful in how they invested, producing profit, and the master placed them over greater things.

We are called to use the talents we have been given for the work of the Lord. Laziness is not good, because it undermines the work of God.

The broader definition is that we are faithful servants of God so that His grace may be with us and enter into eternal life when he returns.

Good day.