MATANGAZO YA USHARIKA
LEO TAREHE 24 JULAI, 2022
NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI
AMRI MPYA NAWAPA, MPENDANE
1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
2. Wageni: Hakuna wageni waliotufikia na vyeti. Matoleo ya Tarehe 17/07/2022
3. Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.
NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:
0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT
Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL
4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. Alhamisi Maombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.
5. Jumapili ijayo tarehe 31/07/2022 tutashiriki Chakula cha Bwana. Washarika tujiandae.
6. Uongozi wa Umoja wa Vijana unapenda kuwatangazia vijana wote kwamba kutakuwa na mkesha wa kusifu na kuabudu Utakao fanyika hapa usharikani tarehe 29/07/2022. kwaya na vikundi mbalimbali vitakuwepo. Vijana wote mnakaribishwa.
7. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA
Kwa mara ya Kwanza tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 20/08/2022
SAA 09:00 ALASIRI
Bw. John Ezekiel Mfugale na Bi. Tumaini Herico
Kwa mara ya Pili tunatangaza Ndoa zitakazofungwa tarehe 06/08/2022
SAA 08:00 MCHANA
Dr. Zephania Dick Peter Gega na Dr. Lilian Willy Mbise
Matangazo mengine ya Ndoa yapo kwenye ubao wa Matangazo.
8. NYUMBA KWA NYUMBA
- Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Mama Korosso
- Mjini kati: watafanya kwa njia ya Mtandao.
- Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Bwana na Bibi James Monyo
- Kinondoni: Kwa Dr. na Bibi T.M. Onesmo
- Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Kwa Bibi Masala Korosso
- Upanga: Watatangaziana
- Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach: Kwa Dr. na Bibi Shoo
Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili
Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki