MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 OKTOBA, 2022    

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

IMANI YAKO IMEKUPONYA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 16/10/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wa kumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. AlhamisiMaombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Kamati ya Afya na Ustawi wa jamii inapenda kuwatangazia kuwa mafundisho ya afya kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa Mwaka wa Kwanza na wa Pili yatafanyika tarehe 19/11/2022 kuanzia saa 2.30 asubuhi mpaka saa 6.00 mchana hapa Usharikani. Wale waliopata Kipaimara wenye umri wa miaka 15 pia wanakaribishwa kwenye mafundisho haya. Wazazi na Walezi mnaombwa kuandikisha watoto watakaohudhuria kwa Parish Worker ili kufanya maandalizi haya.

6. Jumapili ijayo tarehe 30/10/2022 ni sikukuu ya Mavuno. Hivyo ibada itakuwa ni moja itakayoanza saa 2.00 asubuhi. Washarika tujiandae na tuiombee siku hiyo muhimu.

7. Dayosisi ya Mashariki na Pwani kupitia Dawati la Diakonia, Jinsia na makundi Maalum, imeandaa Mkesha wa Wanawake kwa ngazi ya Dayosisi. Mkesha huu utafanyika Jimbo la Kusini katika Usharika wa Kurasini siku ya Ijumaa tarehe 28/10/2022 kuanzia saa 3.00 Usiku. Wanawake wote mnaombwa kuhudhuria kikamilifu mkesha huu. Aidha siku hiyo ya Ijumaa tarehe 28/10/2022 kuanzia saa 3.00 usiku kutakuwa na mkesha wa vijana ngazi ya Dayosisi katika usharika wa Ubungo. Vijana wote mnaombwa kuhudhuria.

8. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 05/11/2022  

SAA 6.00 MCHANA

Bw. Victor Frank Koyanga na Bi. Annansia Godbless Uronu

Matangazo mengine yapo kwenye ubao wa Matangazo.

9. NYUMBA KWA NYUMBA 

  • Masaki na Oyserbay: kwa Bwana na Bibi Mchangila
  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Chrles Lyimo
  • Mjini kati: Kwa Bwana na Bibi Lwaga
  • Ilala, Chang’ombe na Buguruni: Kwa Christina Mange
  •  
  • Tegeta, Kunduchi, Bahari Beach, Ununio: Watatangaziana
  •  
  • Upanga: Kwa Bwana na Bibi Tom Njau

 

Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Kwanza