MATANGAZO YA USHARIKA    

TAREHE 11 DESEMBA, 2022    

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI

BWANA ANAWAFARIJI WATU WAKE

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli. 

2. Wageni: Hakuna mgeni aliyetufikia kwa cheti. 

3. Matoleo ya Tarehe 04/12/2022

Tunamshukuru Mungu aliyetupa afya ya kumwabudu na utayari wakumtolea kwa hiari mali alizotupa kwa kazi yake.

NAMBA YA SADAKA KWA NJIA YA MTANDAO:

0757 391174 - KKKT AZANIA FRONT

Namba ya Wakala M-PESA – 5795794 – KKKT AZANIA FRONT CATHEDRAL

4. Tunapenda kuwakumbusha na kuwakaribisha wote katika ibada zetu siku za jumapili Ibada ya kwanza, inayoendeshwa kwa lugha ya Kiswahili, inayoanza saa 1:00 asubuhi; Ibada ya pili, inayoendeshwa kwa Kiingereza, inayoanza saa 3:00 asubuhi; Ibada ya tatu, inayoendeshwa kwa Kiswahili, inayoanza saa 4:30 asubuhi. vipindi vya kujifunza neno la Mungu hapa Usharikani kila siku za juma. Morning Glory saa 12.00 asubuhi ili kuanza siku kwa Uongozi wa Mungu, Ibada za mchana saa 7.00 -7.30 mchana tunapopata faragha binafsi na Mungu. AlhamisiMaombi na Maombezi saa 11.00 jioni. Vipindi vyote vinarushwa Mubashara kupitia Azania Front TV. Karibu.

5. Jumamosi ijayo tarehe 17 Desemba, 2022 kuanzia saa 10:00 jioni hadi saa 1:00 usiku kutakuwa na Uiwmbaji wa Nyimbo za Krismas (Christmas Carols). Kwaya zetu zote zinazohudumu zetu zote hapa Kanisa Kuu, zitashiriki. Tusiache kuiombea siku hiyo ya jumamosi ifanikiwe. Wote tunakaribishwa kuhudhuria. Mungu awabariki sana.

6. Leo tarehe 11/12/2022 tutamtolea Mungu Fungu la kumi. Washarika karibuni.

7. Uongozi wa Kwaya Kuu ya Usharika unaendelea kuwaomba Wanakwaya wa vikundi vyote kushiriki na kuungana nao kwenye ibada ya Christmas Carols itakayofanyika siku ya ijumaa tarehe 23/12/2022 saa 11.00 jioni Kanisa la St Alban’s Anglican Cathedral. Mazoezi yanaendelea kila siku ya jumanne saa 11.00 jioni. Mungu awawezeshe waimbaji wote kufika kwenye mazoezi na kwa wakati.

8. Shukrani: Jumapili ijayo tarehe 18/12/2022 katika ibada ya Tatu saa 4.30 asubuhi

Familia ya Bwana na Bibi Rodrick Kombe watamshukuru Mungu kwa mambo mengi aliyowatendea ikiwa ni pamoja na mama yao Florah Rodrick Kombe kutimiza miaka 70 ya kuzaliwa kwake mnamo tarehe 25/09/2022.

Neno: Zaburi 106:1-4, Wimbo: TMW 262

9. Huduma ya malezi na makuzi ya watoto Kikristo ya Mjenge Mwanao imeandaa semina ya watoto wa kike na kiume, miaka 12-19, tarehe 17 Disemba 2022, ukumbi wa Anglikana St Alban_posta mpya, ada ni 25,000/=(chai&chakula) Masomo yatakayofundishwa ni Kujitambua ndani ya Kristo, Uwajibikaji na Afya ya Uzazi. Kwa mawasiliano na malipo tumia namba 0757 000151.Tuwapeleke watoto wetu wajifunze na wasaidiwe majibu ya maswali yao kiroho na kitaalamu.

10. NDOA. NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 17/12/2022. NDOA HII ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT NKOARANGA DAYOSISI YA MERU KATI YA

Bw. Urasa Olufemi Sarakikya na Bi. Gloria Nduminsary Swai

PIA NDO HII IFUATAYO ITAFUNGWA USHARIKA WA KKKT NGAYA MOSHI KATI YA 

Bw. Elifuraha Israel lema na Bi. Victoria Benny Sifael

10. NYUMBA KWA NYUMBA 

  • Makumbusho, Kijitonyama, Sinza, Mwenge, Makongo na Ubungo: Kwa Bwana na Bibi Charles Lyimo
  • Kinondoni: Kwa Prof. na Bibi S. Kulaba 
  • Mikocheni, Kawe, Mbezi Beach:Kwa Bwana na Bibi Victor Kida saa 12 jioni

11. Zamu: Zamu za wazee ni Kundi la Pili.

Na huu ndiyo mwisho wa matangazo yetu, Bwana ayabariki.