MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 23 APRILI, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI YESU KRISTO AJIFUNUA KWA WANAFUNZI

  1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.
  1. Wageni: wageni waliotufikia na cheti ni Mrs Patricia Namonje Sinyinza toka United Church of Zambia Usharika wa St. Peter’s Mwenzo
  1. Uongozi wa Umoja wa Wanawake unapenda kuwakumbusha wanawake kuwa tamasha la uimbaji ni tarehe 13.05.2017 mazoezi yanaendelea kila Jumatano saa 10.00 jioni.
  1. Jumapili ijayo tarehe 30/05/2017 katika ibada ya pili Dada Catherine Jengo atamshukuru Mungu kwa kumlinda kwenye ajali aliyopata na kumponya majeraha yote.

Neno: Zaburi 111:1, Wimbo: Kwaya ya Vijana (Namshukuru Mungu)

  1. Mzee Salewi anaomba kukutana na wamachame wote baada ya ibada hapo nje chini ya mti.
  1. Kamati ya Misioni na Uinjilisti kwa niaba ya Uongozi wa Kanisa Kuu Azania Front, inapenda kuwatangazia watu wote kuwa Semina ya NDOA NA FAMILIA kwa siku 9, imeanza jana jumamosi tarehe 22.04.2017 mpaka jumapili tarehe 30.04.2017 kila siku hapa Usharikani Azania Front. Semina hiyo itafundishwa na Mch. Mathias Mushin a Mkewe Jessie Mushi toka KKKT Kaskazini Kati Arusha.  Semina hii itahusu watot, vijana na wanandoa wa kila rika.  Aidha kutakuwa na muda wa maombi na maombezi. 

 

Ratiba ya Semina ni Kama ifuatavyo:

Jumapili 23 April 2017 saa 9.00 alasiri: ufunguzi wa Semina na siku ya kwanza ya Semina

Jumatatu 24 April 2017 - Ijumaa 28 April 2017 saa 11:30 - 1:00 Vipindi vya Semina kwa wanandoa

Jumatano 26 April  2017 saa 4:00 asubuhi Semina kwa Vijana

                                   Saa 9.00 alasiri Wajane na Wagane

                      Saa 11.00-1.30Semina ya Wanandoa na wagane na Wajane

Jumamosi tarehe 29 April 2017 saa 4:00 asubuhi

- watoto wote  - saa 4.00-5.00

- vijana wote   - saa 4.00 – 7.00 mchana

- kwaya zote   - saa  5:30


Jumamosi 29 April 2017 - Jumapili 30 April 2017 saa 9:00 - 12:00 Jioni - Semina ya Wanandoa

Jumapili 30.04.2017, kutakuwa na Sherehe ya wanandoa na kukata keki.

 

Wote mnakaribishwa na muwakaribishe na wengine.
 

  1. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

Kwa mara ya Kwanza tunatangaza ndoa  za tarehe 13/05/2017

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Erick Godian Mwakipesile        na     Bi. Adeline Josephine Mmbaga

SAA 10.00 JIONI

Bw. Ajelandro Mushobozi Sindano na     Bi. Rehema Mahmoud Kikwere

Kwa mara ya Pili tunatangaza ndoa  za tarehe 06/05/2017

SAA 6.00 MCHANA

Bw. Morries Walter Shangali          na     Bi. Elke Norah Sumari

SAA 10.00 JIONI

Bw. Eliah Emmanuel Kinyunyu      na     Bi. Emilia Bonifas Mdamba

Kwa mara ya Tatu tunatangaza ndoa  za tarehe 29/04/2017

SAA 9.00 ALASIRI

Bw. Edson Kakulu Ndanguzi          na     Bi. Gloria Nomsa Labarani

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

  1. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

 

  • Upanga: kwa Bwana na Bibi Kisamo
  • Kinondoni:  Watatangaziana
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Dk na Bibi David Ruhago
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana
  • Oysterbay/Masaki: Watatangaziana
  • Tabata: Watatangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Mama Korosso
  • Mjini kati: Watatangaziana
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio: Watatangaziana

 

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Kwanza.

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.  

 

 

ZAMU ZA WAZEE

IBADA I

Mzee N. Ndosa    - Neno:  Zab. 115:1-10, 1Kor. 15:12-19, Yn: 20:26-29

Mzee N. Masawe - Matangazo

Mzee V. Minja     -  S/School

Mzee S. Jengo    -  Ndoa

                

IBADA II

Mzee Doris Maro   - Neno:  Zab. 115:1-10, 1Kor. 15:12-19, Yn: 20:26-29

Mzee V. MPuya      - Matangazo

Mzee E. Mlaki       - S/School

Mzee E. Nangawe -  Ndoa