MATANGAZO YA USHARIKA

TAREHE 17 SEPTEMBA, 2017

NENO LINALOTUONGOZA SIKU YA LEO NI UWAKILI WETU KWA BWANA

1. Tunawakaribisha wote tumwabudu Mungu wetu katika Roho na kweli.

2. Wageni:  Hakuna mgeni aliyetufikia na cheti.

3. Wiki ijayo kuanzia Jumatatu tarehe 25/09/2017 hadi Jumapili tarehe 01/10/2017  kutakuwa na  semina ambayo  itahusu maombi.  Semina hiyo itaanza saa 11.00 jioni kila siku.  Mwalimu wa semina atakuwa Mchungaji Deogratius Msanya toka KKKT Moshi.  Pia atahudumu wiki nzima katika ibada za asubuhi.  Wote mnakaribishwa.

4. Vitenge vya Miaka mia tano ya matengenezo ya Kanisa vipo.  Vitauzwa hapo nje na viongozi wa Umoja wa Wanawake kwa bei ya sh. 15,000/=.  Aidha Vitenge vya Kiharaka navyo bado vipo, vitauzwa hapo nje kwa bei ya shilingi elf 10.  Washarika karibuni.

5. Jumapili ijayo tarehe 24.09.2017 ni siku ya Harambee ya kituo chetu cha Kiharaka.  Siku hiyo ibada itakuwa ni moja itakayoanza saa 2.00 asubuhi na kuongozwa na Baba Askofu Alex G. Malasusa. Siku hiyo kila msharika avae vazi la kitenge chetu cha Kiharaka. Washarika tuiomboee siku hiyo.

6. Kamati ya Afya na Ustawi wa Jamii Azania Front inapenda kuwashukuru wazazi kwa kuwaleta watoto kwenye semina iliyofanyika jana tarehe 16/09/2017.  Mungu awabariki sana.

7. Leo tutashiriki Chakula cha Bwana.  Washarika karibuni.

8. Jumamosi tarehe 30/09/0217 saa 3.00 asubuhi Kutakuwa na Mkutano wa VICOBA ya Wajane na Wagane wa Azania Front. Wahusika wote wanaombwa kuhudhuria mkutano huo.

9. Ijumaa ijayo tarehe 22/09/2017 saa 11.00 jioni kutakuwa na kikao cha Baraza la Wazee.

 

10. NDOA

NDOA ZA WASHARIKA

KWA MARA YA KWANZA NA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 01/10/2017

SAA 8.00 MCHANA

Bw. Victor Eliazer Mwasele       na    Bi. Anastazia Nicolaus Kampa

 

KWA MARA YA PILI TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 30/09/2017

NDOA HII ITAFUNGA  KANISA LA ANGLIKAN NEEMA CATHEDRAL RUBUNGO

Bw. Jossam Mugisha Mabaraza          na    Bi. Magreth Ernest Mtui

 

KWA MARA YA TATU TUNATANGAZA NDOA ZA TAREHE 23/09/2017

NDOA HII ITAFUNGA  KANISA LA KATOLIKI ST. PETER

Bw. Paul Kennedy Ongoma      na    Bi. Shanga Prize Naomi Jackson Kaale

 

Matangazo mengine ya Ndoa yamebandikwa kwenye ubao wa matangazo Karibu na duka letu la vitabu.

 

11. Ibada za Nyumba kwa Nyumba

  • Upanga: Watatangaziana
  • Kinondoni: Watatangaziana
  • Ilala/Chang’ombe/Mivinjeni: Dada Frida Njowoka
  • Kawe/Mikocheni/Mbezi Beach: Watatangaziana
  • Oysterbay/Masaki: Kwa Judge na Bibi Mlay
  • Tabata: Watatangaziana
  • Kijitonyama/Sinza/Mwenge/Makumbusho/Ubungo: Watatangaziana Mjini kati: Kwa Bibi Victoria Mwansasu
  • Wazo/tegeta/Kunduchi/BahariBeach/Ununio:Kwa Bwana na Bibi Mpuya

Zamu: Zamu za wazee leo ni kundi la Pili

 

Na huu ndio mwisho wa matangazo yetu, Mungu ayabariki.