Date: 
20-04-2022
Reading: 
Marko 16:12-13

Hii ni Pasaka

Jumatano asubuhi tarehe 20.04.2022

Marko 16:12-13

12 Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba.

13 Na hao wakaenda zao wakawapa habari wale wengine; wala hao hawakuwasadiki.

Tembea na Yesu mfufuka;

Marko anaandika kwa kifupi juu ya watu wawili waliokuwa wakielekea shamba, Yesu akaungana nao bila wao kumtambua. Lakini Luka anaandika kwa kirefu ( Soma Luka 24:13-34) kuwa hawakumtambua, wakamwelezea yaliyotokea, na baadaye jioni alipoketi kula nao chakula akajifunua kwao.

Tujiulize; Tunamtambua Yesu? Kielelezo cha kumtambua ni sisi kumpokea, kumsikia na kumfuata. Yesu anajifunua kwetu leo kama mwokozi, akitaka kuingia na kukaa kwetu. Tufungue mioyo yetu, neema hii isitupite kamwe, ndipo tutauona ufalme wake.

Tembea na Yesu mfufuka.

Siku njema.