Date: 
20-01-2022
Reading: 
Marko 1:29-31

Alhamisi asubuhi tarehe 20.01.2022

Marko 1:29-31

29 Na mara walipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana.

30 Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, hawezi homa; na mara wakamwambia habari zake.

31 Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akawatumikia.

Mungu hutakasa nyumba zetu;

Asubuhi ya leo tunaona Yesu akiingia kwa Simoni, na kumponya homa mkwe wa Simoni (mama wa mkewe) aliyekuwa hawezi. Homa ilimwacha mama huyu baada ya kuinuliwa na kushikwa mkono na Yesu.

Baraka ya uponyaji ilipatikana baada ya Yesu kuingia nyumbani mwa Simoni. Kumbe tunawajibika kumkaribisha Yesu nyumbani mwetu, maana ndiye mwenye baraka. 

Siku njema.