Date: 
09-06-2018
Reading: 
Mark 8:35

SATURDAY 9TH JUNE 2018

Mark 8:35

“For whoever wants to save their life will lose it, but whoever loses their life for me and the Gospel will save it”

Let me ask you, as a Christian who loves God, are the things that are important to Jesus becoming increasingly important to you? Whatever the answer, do you know why? Are you enjoying the feeling?
If you have asked Jesus Christ into your life, it is important and necessary then to learn the secrets of living the wondeful life of God, as He had planned for you before the foundation of the world that you should e hoy and without blame before Him in love.
The Bible tells us that it is God’s will that we grow in our relationship with Christ (Ephesians 4:13)and live the tremendous life He planned for us (Ephesians 2:10). You should know that experiencing God is like fitting together pieces of a puzzle! The pieces are;
- The Holy Spirit
- Faith
- God’s Word
- Prayer
- Fellowship, and
- Obedience
Each of the pieces is interellated, and works in conjunction with each other to strengthen our walk with Jesus. The more time you spend understanding and applying what the God’s word says about each piece, the more extreme your life with Christ will become! Are you ready for the Journey?JUMAMOSI TAREHE 6 JUNI 2018

MARKO 8:35


“Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu takayeingamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha” (Mk 8:35)


Nikulize Mkristo unayempenda Mungu, vile vipaumbele vya Yesu, vinaendelea kukua ndani yako na kuwa vyako pia?
Kama umemkaribisha Yesu ndani mwako, basi ni muhimu pia upate kuzijua siri za kuishi maisha mazuri ya Mungu kama alivyotupangia kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili tutengwe kwa ajili yake, tuwe watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Biblia inatuambia kuwa, ni mapenzi ya Mungu kuwa tukue katika mahusiano na Yesu Kristo (Efe 4:13) na kuishi maisha ya utukufu aliyotupangia kwa ajili yetu (Efe 2:10).
Tambua kuwa maisha na Yesu ni sawa na kuwa kila siku unafumbua fumbo la picha yenye sehemu tofauti tofauti, lakini huwezi kuipata hiyo picha bila sehemu zote kuunganishwa pamoja sawasawa. Sehemu hizo ni;
- Roho Mtakatifu
- Imani
- Neno la Mungu
- Maombi
- Ushirika na Mungu
- Utii.
Kila kimoja kinahusiana na kingine na vinafanya kazi katika umoja na kusaidiana katika kuuthibitisha uhusiano wetu na Yesu, kila siku. Na jinsi tunalisoma na kulichunguza Neno la Mungu, linajifunua kwetu na kutufundisha juu ya kila kimoja ya hivi, na ndivyo ushirika wetu na Mungu unavyoimarika na maisha yetu kumwelekea Yesu zaidi. Uko tayari kutebea na Yesu katika safari hii?