Date: 
13-01-2021
Reading: 
Mark 16:14-18

WEDNESDAY 13TH JANUARY 2021  MORNING                                        

Mark 16:14-18 New International Version (NIV)

14 Later Jesus appeared to the Eleven as they were eating; he rebuked them for their lack of faith and their stubborn refusal to believe those who had seen him after he had risen.

15 He said to them, “Go into all the world and preach the gospel to all creation. 16 Whoever believes and is baptized will be saved, but whoever does not believe will be condemned. 17 And these signs will accompany those who believe: In my name they will drive out demons; they will speak in new tongues; 18 they will pick up snakes with their hands; and when they drink deadly poison, it will not hurt them at all; they will place their hands on sick people, and they will get well.”

Jesus calls on believers to trust in Him and through His divine powers, battle evil and be good witnesses of Him. By faith, we have been called to surrender to the Lord’s plan and advance the gospel. How have you personally responded to the call of the Great Commission?


JUMATANO TAREHE 13 JANUARY 2021  ASUBUHI                  

MARKO 16:14-18

14 Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu.
15 Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.
16 Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.
17 Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya;
18 watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.

Yesu anawaita wote wanaomwamini, wamtumaini; na kupitia nguvu zake, wapigane na uovu, halafu kuwa mashahidi wazuri kwa ajili yake. Kwa imani, tumeitwa ili kutii mpango wa Bwana na kuipeleka mbele Injili. Je, wewe umeitikia kwa namna gani wito wa Yesu Kristo wa kuihubiri Injili?