Date: 
20-05-2020
Reading: 
Mark 10:46-52

WEDNESDAY 20TH MAY 2020  MORNING                                                    

Mark 10:46-52  New International Version (NIV)

46 Then they came to Jericho. As Jesus and his disciples, together with a large crowd, were leaving the city, a blind man, Bartimaeus (which means “son of Timaeus”), was sitting by the roadside begging. 47 When he heard that it was Jesus of Nazareth, he began to shout, “Jesus, Son of David, have mercy on me!”

48 Many rebuked him and told him to be quiet, but he shouted all the more, “Son of David, have mercy on me!”

49 Jesus stopped and said, “Call him.”

So they called to the blind man, “Cheer up! On your feet! He’s calling you.” 50 Throwing his cloak aside, he jumped to his feet and came to Jesus.

51 “What do you want me to do for you?” Jesus asked him.

The blind man said, “Rabbi, I want to see.”

52 “Go,” said Jesus, “your faith has healed you.” Immediately he received his sight and followed Jesus along the road.

A believer is someone who believes that Jesus is the Christ, the Son of God. Bartimaeus believed that, even before he was healed of his blindness.

It is with confidence that we may confess ‘that our help is in the name of the Lord, Who made the heavens and the earth.’


JUMATANO TAREHE 20 MEI 2020  ASUBUHI                                             

MARKO 10:46-52

46 Wakafika Yeriko; hata alipokuwa akishika njia kutoka Yeriko, pamoja na wanafunzi wake, na mkutano mkubwa, mwana wa Timayo, Bartimayo, yule mwombaji kipofu, alikuwa ameketi kando ya njia.
47 Naye aliposikia ya kwamba ni Yesu Mnazareti, alianza kupaza sauti yake, na kusema, Mwana wa Daudi, Yesu, unirehemu.
48 Na wengi wakamkemea ili anyamaze, lakini alizidi kupaza sauti, Mwana wa Daudi, unirehemu.
49 Yesu akasimama akasema, Mwiteni. Wakamwita yule kipofu, wakamwambia, Jipe moyo; inuka, anakuita.
50 Akatupa vazi lake, akaruka, akamwendea Yesu.
51 Yesu akamjibu, akamwambia, Wataka nikufanyie nini? Yule kipofu akamwambia, Mwalimu wangu, nataka nipate kuona.
52 Yesu akamwambia, Enenda zako, imani yako imekuponya. Mara akapata kuona; akamfuata njiani.

Mkristo au muumini ni mtu yule anayeamini kuwa Yesu ni Kristo, mwana wa Mungu. Bartimayo aliamini hivyo, hata kabla ya kuponywa kwa kufunguliwa macho yake.

Tunao ujasiri kukiri kuwa msaada wetu unapatikana katika Jina la Bwana, aliyeziumba mbingu na nchi.