Date: 
21-10-2019
Reading: 
Luke 8:43-48

MONDAY 21ST OCTOBER 2019 MORNING  LUKE 8:43-48

Luke 8:43-48 New International Version (NIV)

43 And a woman was there who had been subject to bleeding for twelve years,[c] but no one could heal her. 44 She came up behind him and touched the edge of his cloak, and immediately her bleeding stopped.

45 “Who touched me?” Jesus asked.

When they all denied it, Peter said, “Master, the people are crowding and pressing against you.”

46 But Jesus said, “Someone touched me; I know that power has gone out from me.”

47 Then the woman, seeing that she could not go unnoticed, came trembling and fell at his feet. In the presence of all the people, she told why she had touched him and how she had been instantly healed. 48 Then he said to her, “Daughter, your faith has healed you. Go in peace.”

It does not matter where you sit in church or where you stand in the crowd. Jesus knows your need and He knows the things in your heart; and his healing power can touch your life. His power can change your life forever and end your suffering immediately and permanently.


JUMATATU TAREHE 21 OKTOBA 2019  ASUBUHI  LUKA 8:43-48

43 Na mwanamke mmoja, ambaye ametokwa na damu muda wa miaka kumi na miwili, [aliyekuwa amegharimiwa mali zake zote kwa kuwapa waganga] asipate kuponywa na mtu ye yote,
44 alikwenda nyuma yake, akaugusa upindo wa vazi lake; na mara hiyo kutoka damu kwake kulikoma.
45 Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Basi, watu wote walipokana, Petro alimwambia, Bwana mkubwa, makutano haya wanakuzunguka na kukusonga.
46 Yesu akasema, Mtu alinigusa, maana naona ya kuwa nguvu zimenitoka.
47 Yule mwanamke, alipoona ya kwamba hawezi kusitirika akaja akitetemeka, akaanguka mbele yake, akamweleza mbele ya watu wote sababu yake ya kumgusa, na jinsi alivyoponywa mara.
48 Akamwambia Binti, imani yako imekuponya; enenda zako na amani.

Haijalishi uko wapi, iwe kanisani au kwenye umati wa watu. Yesu anajua hitaji lako, na anajua yaliyo moyoni mwako; na nguvu yake ya uponyaji yaweza kugusa maisha yako. Nguvu yake inao uweza wa kubadilisha maisha yako na kuyaondoa mateso yako yote.