Date: 
23-09-2017
Reading: 
Luke 2:22-24 NIV (Luka 2:22-24)

SATURDAY 23RD SEPTEMBER 2017  MORNING                            

Luke 2:22-24 New International Version (NIV)

Jesus Presented in the Temple

22 When the time came for the purification rites required by the Law of Moses, Joseph and Mary took him to Jerusalem to present him to the Lord 23 (as it is written in the Law of the Lord, “Every firstborn male is to be consecrated to the Lord”[a]), 24 and to offer a sacrifice in keeping with what is said in the Law of the Lord: “a pair of doves or two young pigeons.”[b]

Footnotes:

  1. Luke 2:23 Exodus 13:2,12
  2. Luke 2:24 Lev. 12:8

Joseph and Mary took baby Jesus to the temple according to the Jewish laws and offered to God the required sacrifice. They dedicated Jesus to God.  Notice from Leviticus 12:8 that Joseph and Mary did not have much money otherwise they would have offered a lamb. They were humble and faithful and committed to God.

Let us be faithful in obeying God’s laws and giving our offerings and tithes to Him. Let us not say we can not give because we are poor. Let us also commit our children into God’s hands that they would grow to serve Him.   

JUMAMOSI TAREHE 23 SEPTEMBA 2017 ASUBUHI  

LUKA 2:22-24

22 Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, 
23 (kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana), 
24 wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili. 
 

Yusufu na Maria walimpeleka mtoto mchanga Yesu hekaluni. Walimpeleka pamoja na sadaka kufuatana na amri za Mungu. Hawakuwa na fedha nyingi au wangemtolea Mungu kondoo (tazama Law 12:8). Walikuwa wanyenyekevu na waaminifu.

Sisi pia tunapaswa kuleta watoto wetu kwa Mungu. Tuanapaswa kuwaleta kanisani na kuwafundisha Neno la Mungu. Pia tunapaswa kumtolea Mungu zaka na sadaka. Tusiseme sina pesa. Tumtolee Mungu kwa uaminifu kulingana na uwezo wetu.