Date: 
07-04-2022
Reading: 
Luka 7:40-44

Hii ni Kwaresma 

Alhamisi asubuhi tarehe 07.04.2022

Luka 7:40-44

40 Yesu akajibu akamwambia, Simoni, nina neno nitakalo kukuambia. Akasema, Mwalimu, nena.

41 Akasema, Mtu mmoja mkopeshaji alikuwa na wadeni wawili; mmoja amwia dinari mia tano, na wa pili hamsini.

42 Nao walipokuwa hawana cha kumlipa, aliwasamehe wote wawili. Katika hao wawili ni yupi atakayempenda zaidi?

43 Simoni akajibu akasema, Nadhani ni yule ambaye alimsamehe nyingi. Akamwambia, Umeamua haki.

44 Akamgeukia yule mwanamke, akamwambia Simoni, Wamwona mwanamke huyu? Niliingia nyumbani kwako, hukunipa maji kwa miguu yangu; bali huyu amenidondoshea machozi miguu yangu, na kuipangusa kwa nywele za kichwa chake.

Yesu Kuhani mkuu;

Simoni anaulizwa juu ya waliosamehewa deni, anasema atakayempenda zaidi mdai ni yule aliyesamehewa nyingi. Yesu alikuwa akimwekea mazingira Simoni kutambua haki ya Mungu kwa watu wake, kwa kadri ya matendo yao. Ndiyo maana Yesu anamgeukia mwanamke na kumtangazia msamaha wa dhambi, maana alimtendea Yesu vema kuliko Simoni mwenyewe.

Yesu anapomtangazia msamaha wa dhambi mwanamke aliyekuwa na dhambi anatukumbusha kuwa yeye ndiye mpatanishi wetu na Mungu. Hapa tunakumbushwa kufanya toba, na Yesu yuko tayari kutusamehe dhambi akitupatanisha na Mungu wetu.

Siku njema.