Date: 
18-03-2020
Reading: 
John 9;35-41


WEDNESDAY 18TH MARCH 2020  MORNING                          
John 9:35-41 New International Version (NIV)


35 Jesus heard that they had thrown him out, and when he found him, he said, “Do you believe in the Son of Man?”
36 “Who is he, sir?” the man asked. “Tell me so that I may believe in him.”
37 Jesus said, “You have now seen him; in fact, he is the one speaking with you.”
38 Then the man said, “Lord, I believe,” and he worshiped him.
39 Jesus said,[a] “For judgment I have come into this world, so that the blind will see and those who see will become blind.”
40 Some Pharisees who were with him heard him say this and asked, “What? Are we blind too?”
41 Jesus said, “If you were blind, you would not be guilty of sin; but now that you claim you can see, your guilt remains.

Jesus is the Lord over all creation. He is not limited by space and time. Whatever it is we are going through, He knows.  Jesus does not just know, but He cares. He is concerned about our welfare, both in our temporal existence now in this life, and our eternal welfare in the eternal life that every one of us will have.


JUMATANO TAREHE 18 MACHI 2020  ASUBUHI                              

YOHANA 9:35-41
35 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?
36 Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini?
37 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye.
38 Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia.
39 Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu.
40 Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu?
41 Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa.


Yesu ni Bwana juu ya viumbe vyote. Hafungwi na nyakati wala mahali. Kila tunalolipitia, yeye anajua.  Siyo tu kwamba Yesu anafahamu mahitaji yetu, bali anatujali. Yeye anahusika na mahitaji yetu katika maisha yetu ya muda kwenye ulimwengu huu, na maisha yetu ya milele ambayo kila mmoja wetu ataishi.