Date: 
08-06-2018
Reading: 
John 3:30 ..Continued ( Yohana 3:30..inaendelea)

FRIDAY 8TH JUNE 2018

JOHN 3:30  “He must become greater, I must become less” ……continued.

Yesterday I ended up saying maturity in Christ, tends to transform us to manifest our life purpose on earth to be that of Jesus. Question is how do we determine this? One of the measuring sticks we can use to evaluate whether or not Christ’s purposes have become our purposes is this question; “What is consuming my life?”
“Am I only concerned about matters regarding this temporary world, or do I have an eternal perspective?”
In response I would like to think our lives as consisting of “three T”:
- Time
- Talent, and
- Treasure
How we use the three T’s, is a good indicator of what is important to us.
John the Baptist said, “He (Jesus) must become greater”. As we grow in Jesus, soaking our hearts in the Word of God, he becomes more and more important in our thinking (2Cor 10:5), transforming it, and His agenda becomes the guiding force in our lives. We increasingly delight ourselves in the Lord, rather than the things of the world, and He becomes greater, stronger in our lives, we become weaker, and our lives are hidden with Christ in God, and the choices we make regarding our time, talent, and treasure are dictated by His desires.

IJUMAA TAREHE 8 JUNI 2018

YOHANA 3:30 “Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua” ...inaendelea


Jana nilimalizia kwa kusema kuwa, jinsi tunavyozidi kukua katika kumjua Yesu, mtazamo kuhusu kusudi la maisha yetu hapa duniani hubadilika na kufanana na lile la Yesu. Lakini tuna vigezo gani vya kujipima kuwa tunabadilika hivyo? Njia mojawapo ni kujihoji ni nini kinatawala maisha yetu ya kila siku? Je, nimebanwa na mambo yapitayo ya ulimwengu huu au mawazo yangu yameelekezwa kwenye ufalme wa mbinguni?
Kuna vitu vitatu ambavyo vinaweza kutusaidia kuweka vigezo vya kujihoji!

  • Muda wetu
  • Ufahamu wetu
  • Hazina zetu

Jinsi tunavyovitumia vitu hivi na mwelekeo wake katika maisha yetu, yatakueleza bila shaka kujua maisha yako yanatawaliwa na Yesu, au la.
Yohana Mbatizaji ametusaidia sana kwa hili neno, “Yeye hana budi kuzidi...”. Jinsi tunavyozidi kumjua Yesu na kumpenda, na kusoma na kulijua Neno lake, umuhimu wake katika maisha yetu huongezeka, na fikira na ufahamu wetu hubadilika (2Kor 10:5), na tunakuwa tunamuishia Yeye kwa kila kitu. Furaha yetu inakuwa katika kukua katika kumjua Bwana, tunaachana na mambo ya mwili ambayo hapo awali tuliyaenzi, nafasi yake katika maisha yetu inakua na kila tunachokifanaya ni kwa ajili ya utukufu wake, kwa kuwa anatuongoza katika kila jambo. Uwepo wake katika maisha yetu unakuwa na nguvu na uhai wetu unafichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kinachojitokeza ni kwamba Yesu anapata nguvu katika maisha yetu, na jinsi tunavyotumia muda wetu, ufahamu wetu, na hazina zetu, sasa huongozwa na Yesu mwenyewe.