Date: 
19-07-2021
Reading: 
Jeremiah 31:18-20 (Yeremia)

MONDAY 19TH JULY 2021    MORNING                                              

Jeremiah 31:18-20 New International Version (NIV)

18 “I have surely heard Ephraim’s moaning:
    ‘You disciplined me like an unruly calf,
    and I have been disciplined.
Restore me, and I will return,
    because you are the Lord my God.
19 After I strayed,
    I repented;
after I came to understand,
    I beat my breast.
I was ashamed and humiliated
    because I bore the disgrace of my youth.’
20 Is not Ephraim my dear son,
    the child in whom I delight?
Though I often speak against him,
    I still remember him.
Therefore my heart yearns for him;
    I have great compassion for him,”
declares the Lord.

This is our comfort in affliction that the Lord thinks upon us. God has mercy in store for all who seek him in sincerity. The lower thoughts we have of ourselves, the higher God has of us While we are saying, “surely I cannot be a child of God,” He delights in testifying that we are his children.


JUMATATU TAREHE 19 JULY 2021     ASUBUHI                            

YEREMIA 31:18-20

18 Hakika nimemsikia Efraimu, akijililia hivi, Umeniadhibu, nami nikaadhibika, kama ndama asiyeizoelea nira; unigeuze, nami nitageuzwa; kwa maana wewe u Bwana, Mungu wangu.
19 Hakika baada ya kugeuzwa kwangu, nalitubu; na baada ya kufundishwa kwangu, nalijipiga pajani; nalitahayarika, naam, nalifadhaika, kwa sababu naliichukua aibu ya ujana wangu.
20 Je! Efraimu siye mwanangu mpendwa? Je! Siye mtoto apendezaye? Maana kila nisemapo neno juu yake, ningali nikimkumbuka sana; kwa sababu hiyo moyo wangu unataabika kwa ajili yake; bila shaka nitamrehemu, asema Bwana.

Tunapopitia magumu, tunayo faraja kuwa Bwana anatuwazia mema. Mungu anayo akiba ya neema kwa wale wote wamtafutao kwa moyo wote. Kadiri tunavyojiona hatufai mbele zake, Mungu anatuona kuwa tuna thamani kubwa mbele zake. Tunaposema mioyoni mwetu “hakika mimi sistahili kuwa mtoto wa Mungu,” Yeye hupendezwa na kushuhudia kuwa sisi tu watoto wake.