Date: 
21-11-2019
Reading: 
Jeremiah 25:32-38

THURSDAY 21ST NOVEMBER 2019 MORNING                                        

Jeremiah 25:32-38 New International Version (NIV)

32 This is what the Lord Almighty says:

“Look! Disaster is spreading
    from nation to nation;
a mighty storm is rising
    from the ends of the earth.”

33 At that time those slain by the Lord will be everywhere—from one end of the earth to the other. They will not be mourned or gathered up or buried, but will be like dung lying on the ground.

34 Weep and wail, you shepherds;
    roll in the dust, you leaders of the flock.
For your time to be slaughtered has come;
    you will fall like the best of the rams.[f]
35 The shepherds will have nowhere to flee,
    the leaders of the flock no place to escape.
36 Hear the cry of the shepherds,
    the wailing of the leaders of the flock,
    for the Lord is destroying their pasture.
37 The peaceful meadows will be laid waste
    because of the fierce anger of the Lord.
38 Like a lion he will leave his lair,
    and their land will become desolate
because of the sword[g] of the oppressor
    and because of the Lord’s fierce anger.

God wants Christians to deal with our sins; but if we fail to do so, then we will face the chastening hand of God. The time has come for every Christian to live in constant fellowship with God.


ALHAMISI TAREHE 21 NOVEMBA 2019  ASUBUHI                                

YEREMIA 25:32-38

32 Bwana wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia.
33 Na waliouawa na Bwana siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi.
34 Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.
35 Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka.
36 Sauti ya kilio cha wachungaji, na sauti ya kupiga yowe kwao walio hodari katika kundi, kwa maana Bwana anayaharibu malisho yao.
37 Na mazizi yenye amani yamenyamazishwa, kwa sababu ya hasira kali ya Bwana.
38 Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali.

Mungu anataka kila Mkristo atambue na kutubu dhambi zake; lakini tukishindwa kufanya hivyo, mkono wa Mungu utakuwa juu yetu. Wakati umefika kwa kila Mkristo kujenga mahusiano ya kudumu na Mungu.