Date: 
29-04-2022
Reading: 
Isaya 52:7-10

Ijumaa asubuhi tarehe 29.04.2022

Isaya 52:7-10

7 Jinsi ilivyo mizuri juu ya milima Miguu yake aletaye habari njema, Yeye aitangazaye amani, Aletaye habari njema ya mambo mema, Yeye autangazaye wokovu, Auambiaye Sayuni, Mungu wako anamiliki!

8 Sauti ya walinzi wako! Wanapaza sauti zao, wanaimba pamoja; Maana wataona jicho kwa jicho, Jinsi Bwana arejeavyo Sayuni.

9 Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa Bwana amewafariji watu wake, Ameukomboa Yerusalemu.

10 Bwana ameweka wazi mkono wake mtakatifu Machoni pa mataifa yote; Na ncha zote za dunia Zitauona wokovu wa Mungu wetu.

Yesu Kristo ajifunua kwetu;

Isaya anawasihi Israeli kumsifu Bwana kwa sababu ya kuwakomboa. Bwana aliwatoa Yerusalemu kwenye ukiwa na kuwafariji. Katika mstari wa 10, Nabii Isaya anatoa ahadi ya Mungu kutowaacha watu wake, ya kwamba watauona wokovu wake.

Nasi katika majira haya ya Pasaka, tunaitwa kumsifu Mungu kwa ajili ya zawadi ya wokovu kwa njia ya kufa msalabani na kufufuka. Kwa njia ya kifo chake, Yesu ameahidi kutotuacha milele, na ametuhakikishia kuwa tutauona wokovu wake. Umempokea?

Siku njema.