Date: 
17-09-2021
Reading: 
Isaya 41:11-13 (Isaiah)

IJUMAA TAREHE 19 SEPTEMBA 2021, ASUBUHI

Isaya 41:11-13

11 Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.

12 Utawatafuta wala hutawaona wale wapiganao nawe; watakuwa si kitu; watakuwa kama kitu kisichokuwa, wale waliofanya vita juu yako.

13 Kwa maana mimi, BWANA, Mungu wako, nitakushika mkono wako wa kuume, nikikuambia, Usiogope; mimi nitakusaidia.

Mungu hujishughulisha na mambo yetu;

Mungu anaahidi kuwa msaada kwa Taifa lake, yaani Israeli. Anaahidi kuwaepusha na wote waonao hasira juu yao. Kwa kuweka msisitizo, Bwana  anasema "usiogope, mimi nitakusaidia"

Ahadi hii inadumu kwetu hadi leo hii. Mungu ndiye msaada kwetu wakati wote;

Zaburi 46:1

 1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Mungu anapokuwa msaada wetu, maana yake ndiye hutuwezesha katika hali zote. Kwa sababu yeye ni msaada, basi tuendelee kumtegemea yeye ambaye hujishughulisha na mambo yetu.

Ijumaa njema


FRIDAY 17TH SEPTEMBA 2021, MORNING

Isaiah 41:11-13

1 “All who rage against you
    will surely be ashamed and disgraced;
those who oppose you
    will be as nothing and perish.
12 Though you search for your enemies,
    you will not find them.
Those who wage war against you
    will be as nothing at all.
13 For I am the Lord your God
    who takes hold of your right hand
and says to you, Do not fear;
    I will help you.

Read full chapter

God promises to be a help to His people, Israel. He promises to spare them and all who are angry with them. With emphasis, the Lord says "do not be afraid, I will help you"

This promise remains for us to this day. God is our helper at all times;

Psalm 46: 1

 1 God is our refuge and strength, a very present help in trouble. Support that will be abundant in times of persecution.

When God is our help, it means He is the one who empowers us in all situations. Because he is our helper, let us continue to rely on Him who cares for us.

Good Friday