Date: 
09-03-2021
Reading: 
Isaiah 45:9-13

TUESDAY 9th MARCH 2021 MORNING 

Isaiah 45:9-13 New International Version (NIV)

9 “Woe to those who quarrel with their Maker,

    those who are nothing but potsherds

    among the potsherds on the ground.

Does the clay say to the potter,

    ‘What are you making?’

Does your work say,

    ‘The potter has no hands’?

10 Woe to the one who says to a father,

    ‘What have you begotten?’

or to a mother,

    ‘What have you brought to birth?’

11 “This is what the Lord says—

    the Holy One of Israel, and its Maker:

Concerning things to come,

    do you question me about my children,

    or give me orders about the work of my hands?

12 It is I who made the earth

    and created mankind on it.

My own hands stretched out the heavens;

    I marshaled their starry hosts.

13 I will raise up Cyrus[b] in my righteousness:

    I will make all his ways straight.

He will rebuild my city

    and set my exiles free,

but not for a price or reward,

    says the Lord Almighty.”

 

Each one of us is special to God. He loves us and he created us with a particular purpose in mind. God chooses different people as his vessels to do his work. God makes us in a certain way, with certain emotions, and he gives us certain gifts; not by accident, but because God has a certain role for us to play in his world.


JUMANNE TAREHE 9 MACHI 2021 ASUBUHI ISAYA 45:9-13

9 Ole wake ashindanaye na Muumba wake! Kigae kimoja katika vigae vya dunia! Je! Udongo umwambie yeye aufinyangaye; Unafanya nini? Au kazi yako, Hana mikono?

10 Ole wake amwambiaye baba yake, Wazaa nini? Au mwanamke, Una utungu wa nini?

11 Bwana, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni.

12 Mimi nimeiumba dunia, nimemhuluku mwanadamu juu yake; Mimi, naam, mikono yangu mimi, imezitanda mbingu, na jeshi lake lote nimeliamuru.

13 Mimi nimemwinua katika haki, nami nitazinyosha njia zake zote; ataujenga mji wangu, naye atawaacha huru watu wangu waliohamishwa, si kwa kulipwa fedha, wala kwa kupewa zawadi, asema Bwana wa majeshi.

 

Kila mmoja wetu ana umuhimu mbele za Mungu. Yeye anatupenda na alituumba kwa kusudi maalum ndani yake. Mungu huwachagua watu tofauti kama vyombo vyake kuitenda kazi yake. Mungu ametuumba kwa namna ya pekee, kwa tabia tofauti; na ametupa karama tofauti, siyo kwa bahati mbaya, bali ni kwa sababu Yeye analo kusudi kwa kila mmoja wetu kutimiza katika duna hii.