Date: 
30-04-2020
Reading: 
Isaiah 40:10-11

THURSDAY 30TH APRIL 2020  MORNING                                                            

Isaiah 40:10-11 New International Version (NIV)

10 See, the Sovereign Lord comes with power,
    and he rules with a mighty arm.
See, his reward is with him,
    and his recompense accompanies him.
11 He tends his flock like a shepherd:
    He gathers the lambs in his arms
and carries them close to his heart;
    he gently leads those that have young.

Our Lord Jesus is a shepherd who not only leads us but also goes with us on our way tenderly, feeding and caring for our needs. God who holds all of creation in his hand is the same Lord whom we are calling upon His Name, to intervene and deliver us from the COVID-19 pandemic. In Isaiah 43:1b God reminds us saying, “Do not fear, for I have redeemed you; I have summoned you by name; you are mine.”


ALHAMISI TAREHE 30 APRILI 2020  ASUBUHI                                                 

ISAYA 40:10-11

10 Tazameni, Bwana Mungu atakuja kama shujaa, Na mkono wake ndio utakaomtawalia; Tazameni, thawabu yake i pamoja naye, Na ijara yake i mbele zake.
11 Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya wana-kondoo mikononi mwake; Na kuwachukua kifuani mwake, Nao wanyonyeshao atawaongoza polepole.

Bwana wetu Yesu Kristo ni Mchungaji ambaye siyo tu anatuchunga bali huenda nasi katika njia zetu kwa upole, akitulisha na kutupa mahitaji yetu. Mungu anayeutunza uumbaji katika mkono wake, ndiye Bwana yule yule tunayeliitia jina lake, ili apate kuingilia kati na kutuokoa na janga hili la COVID – 19. Katika kitabu hiki cha nabii Isaya 43:1b Mungu anatukumbusha akisema, “Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.”