Date: 
27-01-2022
Reading: 
Hesabu 24:12-16

Alhamisi asubuhi, tarehe 27.01.2022

Hesabu 24:12-16

12 Balaamu akamwambia Balaki, Je! Sikuwaambia wajumbe wako ulionipelekea, nikisema,

13 Kama Balaki angenipa nyumba yake imejaa fedha na dhahabu, siwezi kupita mpaka wa neno la Bwana, kutenda neno jema, wala neno baya, kwa nia yangu mwenyewe; Bwana atakalolinena ndilo nitakalolinena mimi.

14 Basi sasa, tazama, ninakwenda kwa watu wangu; haya, nitakuarifu mambo ambayo watu hawa watakayowatenda watu wako siku za mwisho.

15 Akatunga mithali yake akasema, Balaamu mwana wa Beori asema, Yule mtu aliyefumbwa macho asema,

16 Asema, yeye asikiaye maneno ya Mungu, Na kuyajua maarifa yake Aliye Juu. Yeye aonaye maono ya Mwenyezi, Akianguka kifudifudi, amefumbuliwa macho,

Mungu anaondoa ubaguzi;

Tunasoma habari za Balaamu akimkumbusha Balaki ujumbe aliomtumia awali, kuwa hata angepewa nyumba imejaa fedha na dhahabu, yeye bado angeongozwa na neno la BWANA. Huu ni mfano halisi wa msimamo usioyumba katika kutetea imani. 

Njia ya ufalme wa Mungu siyo nyepesi. Ndiyo maana ni rahisi kwa wengi wetu kuahirisha kwenda ibadani kwa sababu tu mvua inanyesha, lakini tukawa tayari kunyeshewa kwenda kazini! Mungu tunampa nafasi gani? Yeye alishatuokoa, na anasema hana ubaguzi. Sisi tunampa nafasi gani?

Siku njema.