Date: 
04-04-2017
Reading: 
Genesis 14:8-16 (NIV)

TUESDAY 4TH APRIL 2017 MORNING                                      

Genesis 14:8-16  New International Version (NIV)

Then the king of Sodom, the king of Gomorrah, the king of Admah, the king of Zeboyim and the king of Bela (that is, Zoar) marched out and drew up their battle lines in the Valley of Siddim against Kedorlaomer king of Elam, Tidal king of Goyim, Amraphel king of Shinar and Arioch king of Ellasar—four kings against five. 10 Now the Valley of Siddim was full of tar pits, and when the kings of Sodom and Gomorrah fled, some of the men fell into them and the rest fled to the hills. 11 The four kings seized all the goods of Sodom and Gomorrah and all their food; then they went away. 12 They also carried off Abram’s nephew Lot and his possessions, since he was living in Sodom.

13 A man who had escaped came and reported this to Abram the Hebrew. Now Abram was living near the great trees of Mamre the Amorite, a brother[a] of Eshkol and Aner, all of whom were allied with Abram.14 When Abram heard that his relative had been taken captive, he called out the 318 trained men born in his household and went in pursuit as far as Dan. 15 During the night Abram divided his men to attack them and he routed them, pursuing them as far as Hobah, north of Damascus.16 He recovered all the goods and brought back his relative Lot and his possessions, together with the women and the other people.

Footnotes:

  1. Genesis 14:13 Or a relative; or an ally

God was with Abram as he fought the enemies. God gave Abram victory and enabled him to rescue his relative Lot.

Our battle is not physical but spiritual. We fight against Satan and the powers of darkness. Let us seek God’s help and guidance every day. Let us not depend upon our own wisdom and resources but commit all our ways into God’s hands.

JUMANNE TAREHE 4 APRILI 2017 ASUBUHI                             

MWANZO 14:8-16

8 Mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, na mfalme wa Adma, na mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakatoka wakapanga vita panapo bonde la Sidimu; 
9 wapigane na Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, na Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, wafalme wanne juu ya wale watano. 
10 Na bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami. Nao wafalme wa Sodoma na Gomora wakakimbia, wakaanguka huko, nao waliosalia wakakimbia milimani. 
11 Wakachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, wakaenda zao. 
12 Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao. 
13 Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; naye amekaa panapo mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu. 
14 Abramu aliposikia ya kwamba nduguye ametekwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani. 
15 Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski. 
16 Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu. 
 

Mungu alikuwa pamoja na Abramu wakati vita. Mungu alimpa ushindi dhidi ya maadui zake na alimwezesha kumwokoa ndugu yake Lutu na mali zake.

Vita yetu si ya kimwili, bali tuna vita ya kiroho dhidi ya Shetani na nguvu za giza. Tuvae silaha zote za roho na tutafute msaada na uongozi wa Mungu kila siku. Mungu atatubariki na kutuwezesha katika yote.