Date: 
18-01-2020
Reading: 
Ezikiel 36:22-28

SATURDAY 18TH JANUARY 2020  MORNING                                                    
Ezekiel 36:22-28 New International Version (NIV)
22 “Therefore say to the Israelites, ‘This is what the Sovereign Lord says: It is not for your sake, people of Israel, that I am going to do these things, but for the sake of my holy name, which you have profaned among the nations where you have gone. 23 I will show the holiness of my great name, which has been profaned among the nations, the name you have profaned among them. Then the nations will know that I am the Lord, declares the Sovereign Lord, when I am proved holy through you before their eyes.
24 “‘For I will take you out of the nations; I will gather you from all the countries and bring you back into your own land. 25 I will sprinkle clean water on you, and you will be clean; I will cleanse you from all your impurities and from all your idols. 26 I will give you a new heart and put a new spirit in you; I will remove from you your heart of stone and give you a heart of flesh. 27 And I will put my Spirit in you and move you to follow my decrees and be careful to keep my laws. 28 Then you will live in the land I gave your ancestors; you will be my people, and I will be your God. 


The human heart is the centre of personality, the source of every thought, and the fountain of the will.
A transformed humanity will channel God's holiness and witness to God's glory among the nations.
    


JUMAMOSI TAREHE 18 JANUARI 2020  ASUBUHI                                    
EZEKIEL 36:22-28
22 Kwa hiyo; waambieni nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi Sitendi hili kwa ajili yenu, Ee nyumba ya Israeli, bali kwa ajili ya jina langu takatifu, mlilolitia unajisi katika mataifa mliyoyaendea.
23 Nami nitalitakasa jina langu kuu, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, asema Bwana MUNGU, nitakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao.
24 Maana nitawatwaa kati ya mataifa, nami nitawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.
25 Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote.
26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama.
27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.
28 Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.

Moyo wa mwanadamu ndiyo asili ya utu wake, ni asili ya mawazo yake yote; na chemichemi ya utashi wake.
Moyo uliofanywa upya na Mungu utakuwa mahali patakatifu pa Mungu na kuutangaza utukufu wa Mungu kwa mataifa.