Date: 
22-09-2017
Reading: 
Exodus 35:20-29 NIV (Kutoka 35:20-29)

FRIDAY  22ND SEPTEMBER 2017 MORNING                           

Exodus 35:20-29 New International Version (NIV)

20 Then the whole Israelite community withdrew from Moses’ presence,21 and everyone who was willing and whose heart moved them came and brought an offering to the Lord for the work on the tent of meeting, for all its service, and for the sacred garments. 22 All who were willing, men and women alike, came and brought gold jewelry of all kinds: brooches, earrings, rings and ornaments. They all presented their gold as a wave offering to the Lord. 23 Everyone who had blue, purple or scarlet yarn or fine linen, or goat hair, ram skins dyed red or the other durable leather brought them. 24 Those presenting an offering of silver or bronze brought it as an offering to the Lord, and everyone who had acacia wood for any part of the work brought it. 25 Every skilled woman spun with her hands and brought what she had spun—blue, purple or scarlet yarn or fine linen. 26 And all the women who were willing and had the skill spun the goat hair. 27 The leaders brought onyx stones and other gems to be mounted on the ephod and breastpiece. 28 They also brought spices and olive oil for the light and for the anointing oil and for the fragrant incense. 29 All the Israelite men and women who were willing brought to the Lord freewill offerings for all the work the Lord through Moses had commanded them to do.

It is important to give to God’s work.  Notice that the people obeyed Moses’ call to give an offering to the Lord. They also gave willingly not resenting the offering. They also gave the best they had not just leftovers. They used their skills to produce beautiful items.

Let us give to God joyfully willingly. Let us use our time and talents and money and possessions in God’s service. Let us be thankful for all the blessings that God has given to us.

IJUMAA TAREHE 22 SEPTEMBA 2017 ASUBUHI                         

KUTOKA 35:20-29

20 Basi mkutano wote wa wana wa Israeli wakaondoka hapo mbele ya Musa. 
21 Wakaja kila mtu ambaye moyo wake ulimhimiza, na kila mtu ambaye roho yake ilimfanya kuwa apenda, nao wakaleta sadaka za kumpa Bwana, kwa kazi ya hema ya kukutania, na kwa utumishi wake, na kwa hayo mavazi matakatifu. 
22 Nao wakaja, waume kwa wake, wote waliokuwa na moyo wa kupenda, wakaleta vipini, na hazama, na pete za muhuri, na vikuku, na vyombo vyote vya dhahabu; kila mtu aliyetoa toleo la dhahabu la kumpa Bwana. 
23 Tena kila mtu aliyeona kwake nyuzi za rangi ya samawi, na nyuzi za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri, na singa za mbuzi, na ngozi za kondoo waume zilizotiwa rangi nyekundu, na ngozi za pomboo, akavileta. 
24 Kila mtu aliyetoa toleo la fedha, na la shaba, akaileta sadaka ya Bwana; na kila mtu, aliyeona kwake mti wa mshita kwa kazi yo yote ya huo utumishi, akauleta. 
25 Na wanawake wote waliokuwa na mioyo ya hekima, walisokota kwa mikono yao, nao wakaleta hizo walizokuwa wamezisokota, nguo za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na hizo nyuzi nyekundu, na hiyo nguo ya kitani nzuri. 
26 Na wanawake wote ambao mioyo yao iliwahimiza katika hekima wakasokota hizo singa za mbuzi. 
27 Na hao wakuu wakavileta vile vito vya shohamu, na vito vya kutiwa, kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani, 
28 na viungo vya manukato, na mafuta; kwa hiyo taa, na kwa hayo mafuta ya kutiwa, na kwa huo uvumba mzuri. 
29 Wana wa Israeli wakaleta sadaka za kumpa Bwana kwa moyo wa kupenda; wote, waume kwa wake, ambao mioyo yao iliwafanya kuwa wapenda kuleta kwa hiyo kazi, ambayo Bwana aliamuru ifanywe kwa mkono wa Musa. 

Ni vema kumtolea Mungu sadaka. Watu waliitikia wito wa Musa kumtolea Mungu sadaka. Pia walitoa sadaka kwa hiari bila kulazimishwa. Walitoa sadaka iliyo bora na ya thamani. Walitumia vipawa vyo kutengeneza vitu vizuri.

Tumtolee  Mungu sadaka njema kwa hiari. Tumshukuru Mungu kwa baraka nyingi alizotupa na tumtolee sadaka nzuri.