Date: 
25-01-2021
Reading: 
Exodus 34:29-35 (Kutoka 34:29-35)

MONDAY 25TH JANUARY 2021     MORNING                                                 

Exodus 34:29-35  New International Version (NIV)

29 When Moses came down from Mount Sinai with the two tablets of the covenant law in his hands, he was not aware that his face was radiant because he had spoken with the Lord. 30 When Aaron and all the Israelites saw Moses, his face was radiant, and they were afraid to come near him. 31 But Moses called to them; so Aaron and all the leaders of the community came back to him, and he spoke to them. 32 Afterward all the Israelites came near him, and he gave them all the commands the Lord had given him on Mount Sinai.

33 When Moses finished speaking to them, he put a veil over his face. 34 But whenever he entered the Lord’s presence to speak with him, he removed the veil until he came out. And when he came out and told the Israelites what he had been commanded, 35 they saw that his face was radiant. Then Moses would put the veil back over his face until he went in to speak with the Lord.

God’s light shines through the actions and lives of leaders and ordinary people of faith, to make God’s transforming presence known in the congregation and wider community.


JUMATATU  TAREHE 25 JANUARY 2021      ASUBUHI                              

KUTOKA 34:29-35

29 Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling'aa kwa sababu amesema naye.
30 Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake iling'aa; nao wakaogopa kumkaribia.
31 Musa akawaita; Haruni na wakuu wote wa kusanyiko wakarudi kwake; Musa akasema nao.
32 Baadaye wana wa Israeli wote wakakaribia; akawausia maneno yote ambayo Bwana amemwambia katika mlima Sinai.
33 Na Musa alipokuwa amekwisha kusema nao, akatia utaji juu ya uso wake.
34 Lakini desturi ya Musa ilikuwa alipoingia mbele za Bwana kusema naye, kuuvua huo utaji mpaka atoke; akatoka akawaambia wana wa Israeli maneno yote aliyoambiwa.
35 Wana wa Israeli wakauona uso wa Musa ya kuwa ngozi ya uso wake Musa iling'aa; naye Musa akautia utaji juu ya uso wake tena, hata alipoingia kusema naye.

Nuru ya Mungu hung’aa kupitia matendo na maisha ya viongozi na watu wa kawaida wenye imani, ili kufanya uwepo wa Mungu kujulikana katika kanisa na jamii yote.