Date: 
05-02-2020
Reading: 
Exodus 3:1-6 (Kutoka 3:1-6)

TUESDAY 4TH FEBRUARY 2020  MORNING                                                                                

Exodus 3:1-6 New International Version (NIV)

1 Now Moses was tending the flock of Jethro his father-in-law, the priest of Midian, and he led the flock to the far side of the wilderness and came to Horeb, the mountain of God. There the angel of the Lord appeared to him in flames of fire from within a bush. Moses saw that though the bush was on fire it did not burn up. So Moses thought, “I will go over and see this strange sight—why the bush does not burn up.”

When the Lord saw that he had gone over to look, God called to him from within the bush, “Moses! Moses!”

And Moses said, “Here I am.”

“Do not come any closer,” God said. “Take off your sandals, for the place where you are standing is holy ground.” Then he said, “I am the God of your father,[a] the God of Abraham, the God of Isaac and the God of Jacob.” At this, Moses hid his face, because he was afraid to look at God.

God dwells in us, and so we shall live as long as He lives. He has called us for the special purpose to accomplish His plan. The fire that He puts in our heart shall be a fountain of fire springing up into life everlasting.


JUMANNE TAREHE 4 FEBRUARI 2020                                           

ASUBUHI  KUTOKA 3:1-6

1 Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
Malaika wa Bwana akamtokea, katika mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti; akatazama, na kumbe! Kile kijiti kiliwaka moto, nacho kijiti hakikuteketea.
Musa akasema, Nitageuka sasa, niyaone maono haya makubwa, na sababu kijiti hiki hakiteketei.
Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame, Mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti, akasema, Musa! Musa! Akasema, Mimi hapa.
Naye akasema, Usikaribie hapa; vua viatu vyako miguuni mwako; maana mahali hapo unaposimama ni nchi takatifu.
Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akaficha uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.

Mungu anakaa ndani yetu, hivyo tunapaswa kuishi ndani yake nyakati zote. Mungu ametuita kwa kusudi maalum ili kutimiza mpango wake. Moto aliowasha ndani ya mioyo yetu utakuwa chemichemi itakayoenea hata uzima wa milele.