Date: 
13-03-2017
Reading: 
Exodus 2:11-15 (NIV)

MONDAY 13TH MARCH 2017 MORNING                                     

Exodus 2:11-15  New International Version (NIV)

Moses Flees to Midian

11 One day, after Moses had grown up, he went out to where his own people were and watched them at their hard labor. He saw an Egyptian beating a Hebrew, one of his own people. 12 Looking this way and that and seeing no one, he killed the Egyptian and hid him in the sand. 13 The next day he went out and saw two Hebrews fighting. He asked the one in the wrong, “Why are you hitting your fellow Hebrew?”

14 The man said, “Who made you ruler and judge over us? Are you thinking of killing me as you killed the Egyptian?” Then Moses was afraid and thought, “What I did must have become known.”

15 When Pharaoh heard of this, he tried to kill Moses, but Moses fled from Pharaoh and went to live in Midian, where he sat down by a well.

In these few verses we read of several examples of violence and discrimination. Often violence breeds violence. One violent act leads to another.

If we feel that we or our loved ones have been badly treated we may react violently to those involved. May God help us to treat everyone with respect and consideration and to work towards peaceful solutions to conflicts.

JUMATATU TAREHE 13 MACHI 2017 ASUBUHI                       

KUTOKA 2:11-15

11 Hata siku zile, Musa alipokuwa mtu mzima, akatoka kuwaendea ndugu zake, akatazama mizigo yao. Akamwona Mmisri anampiga Mwebrania, mmojawapo wa ndugu zake. 
12 Basi akatazama huko na huko, na alipoona ya kuwa hapana mtu, akampiga Mmisri yule, akamficha ndani ya mchanga. 
13 Akatoka siku ya pili, na tazama, watu wawili wa Waebrania walikuwa wakipigana. Akamwambia yule aliyemdhulumu mwenzake, Mbona unampiga mwenzako? 
14 Yule akasema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu wetu, na mwamuzi juu yetu? Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri? Musa akaogopa, akasema, Kumbe! Jambo lile limejulikana. 
15 Basi Farao alipopata habari, akataka kumwua Musa; lakini Musa akakimbia mbele ya Farao, akakaa katika nchi ya Midiani; akaketi karibu na kisima. 
 

Katika mistari hii michache tunasoma mifano ya ukatili. Mara nyingi tendo moja la ukatili linasababisha lingine na lingine, kila mtu akilipa kisasi kwa mwingine.

Tumwombe Mungu tusiwe watu wakatili, bali tuheshimu na tumhurumie kila mtu na tutafute suluhisho kwa amani katika watu au jamii zinazogombana.