Date: 
11-06-2018
Reading: 
Ephesians 4:23 (Waefeso 4:23)

MONDAY 11TH JUNE 2018

Ephesians 4:23


“Be renewed in the spirit of your mind” (Eph 4:23)


Many Christians is something old. No fresh stream of living water flows through their heart. Prayer has become only a habit, and the reading of the Word a merely empty form. There is no fire from within them! No initiative! No sense of need and no joy of salvation. There is no burning in their hearts when the Word of God is spoken to them. Their whole Christian life has become stiff and stereotype! There is a hard shell and within the shell is nothing but emptiness. But thanks to God in Jesus Christ that there is power and a way to make a new beginning!
Jesus says;
“Be renewed in the spirit of your mind”
Incidentally, by saying, “renewal in the spirit”, it means, this renewal must come from within. The mere intention to become new is not enough. Know that it is from within your mind that you wither and die, and it is also from there that a new life must begin and spring up and make a fresh beginning. However, it is God alone who is able to give you that. Go to Him! Humble yourself! When you truly humble yourself to him he will transform and renew  you through and through and impart in your mind which was also in Christ Jesus. Keep on asking Him to sustain that renewal day by day.



JUMATATU TAREHE 11 JUNI 2018

WAEFESO 4:23

“Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu” (Efe 4:23)


Wakristo wengi hawaishi maisha mapya. Hakuna mito ya maji yenye baraka itokayo katika maisha yao. Maombi kwao kimekuwa kitu cha desturi tu, na hata wakisoma Neno la Mungu, hawaoni uwepo wowote wa Mungu! Hawana nguvu za ki-Mungu ndani yao tena, wala vifua vyao haviwaki moto wakilisikia Neno la Mungu, hakuna msukumo wala hamu ya kuutafuta uso wa Mungu. Maisha yao yote ya Ki-Kikristo yamekuwa hayana mabadiliko wala hayatofautiani na wale wasioamini. Ni kama wamefungwa na ndani mwao hakuna nguvu tena ya kubadilika. Lakini ashukuriwe Mungu katika Kristo Yesu ambaye ndani mwake tunapata nguvu mpya na ya mabadiliko.
Yesu anasema; “mfanywe wapya katika roho ya nia zenu”
Kamata hiki, “Upya unaotoka katika roho ya nia zetu”, yaani upya huu lazima uanzie ndani mwetu. Kuwa tu na mpango wa kubadilika hakutoshi, lazima kuwe na hatua za kutaka mabadiliko. Jua kwamba kusinyaa na kufa kwa nia kulianzia ndani mwako, katika nafsi yako; kadhalika na kufanywa upya lazima kuanzie nafsini, machipuko mapya yaanzie huko. Bila hivyo hakuna mabadiliko. Na ni Mungu pekee ndiye anayeweza kukubadilisha. Yeye anakuita uende kwake, sasa! Nenda! Jinyenyekeze katika mkono wake ulio hodari. Na ukijinyenyekeza kwa kweli na kuutafuta uso wake kwa bidii, atakubadilisha, na kukufanya upya kuanzia kwenye nia yako. Atakupa nia ile ile ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu! Na uendelee hivyo kumtafuta kila siku, naye ataendelea kukufanya upya siku hadi siku.