Date: 
11-06-2019
Reading: 
Ephesians 4:11-16 (Efeso 4:11-16)

TUESDAY 11TH JUNE 2019 MORNING                                           

Ephesians 4:11-16 New International Version (NIV)

11 So Christ himself gave the apostles, the prophets, the evangelists, the pastors and teachers, 12 to equip his people for works of service, so that the body of Christ may be built up 13 until we all reach unity in the faith and in the knowledge of the Son of God and become mature, attaining to the whole measure of the fullness of Christ.

14 Then we will no longer be infants, tossed back and forth by the waves, and blown here and there by every wind of teaching and by the cunning and craftiness of people in their deceitful scheming. 15 Instead, speaking the truth in love, we will grow to become in every respect the mature body of him who is the head, that is, Christ. 16 From him the whole body, joined and held together by every supporting ligament, grows and builds itself up in love, as each part does its work.

God is still working in His church today through the power of the Holy Spirit. God has raised up leaders with different spiritual gifts to lead His church. It is God’s will that we all become mature in Christ. We also need to be united in love as we work together for God’s glory.

Ask God to show you what is your role in His church.


JUMANNE TAREHE 11 JUNI 2019 ASUBUHI                                    

EFESO 4:11-16

11 Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 
12 kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 
13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 
14 ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 
15 Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 
16 Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo. 
 

Mungu bado hufanyakazi katika kanisa lake kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Mungu ameinua watu wenye vipawa mbalimbali kuongoza kanisa lake. Lengo la Mungu ni sisi sote tukue kiroho. Pia tufanye kazi pamoja kwa upendo na kwa utukufu wa Mungu.

Mwombe Mungu akuonyeshe Nafasi yako katika kanisa lake.