Date: 
03-03-2020
Reading: 
Ecclesiastes 7:4-11 (Mhubiri 7:4-11)

TUESDAY 3RD MARCH 2020   MORNING                                                  

Ecclesiastes 7:4-11 New International Version (NIV)

The heart of the wise is in the house of mourning,
    but the heart of fools is in the house of pleasure.
It is better to heed the rebuke of a wise person
    than to listen to the song of fools.
Like the crackling of thorns under the pot,
    so is the laughter of fools.
    This too is meaningless.

Extortion turns a wise person into a fool,
    and a bribe corrupts the heart.

The end of a matter is better than its beginning,
    and patience is better than pride.
Do not be quickly provoked in your spirit,
    for anger resides in the lap of fools.

10 Do not say, “Why were the old days better than these?”
    For it is not wise to ask such questions.

11 Wisdom, like an inheritance, is a good thing
    and benefits those who see the sun.

Despite the fact that that our life seems to be filled with difficult things, difficult people, difficult situations, problems that are beyond our ability, the preacher asserts that they are more valuable than the pleasant things that you and I prefer to experience.


JUMANNE TAREHE 3 FEBRUARI 2020  ASUBUHI                                      

MHUBIRI 7:4-11

Moyo wake mwenye hekima umo nyumbani mwa matanga, bali moyo wake mpumbavu umo nyumbani mwa furaha.
Heri kusikia laumu ya wenye hekima, Kuliko mtu kusikia wimbo wa wapumbavu;
Maana kama mlio wa miiba chini ya sufuria, Ndivyo kilivyo kicheko cha mpumbavu. Hayo nayo ni ubatili.
Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima, Na rushwa huuharibu ufahamu.
Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake, Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.
Usifanye haraka kukasirika rohoni mwako, Maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
10 Usiseme, Kwani siku za kale kupita siku hizi? Maana si kwa hekima uulizavyo neno hilo.
11 Hekima ni njema, mfano wa urithi; Naam, nayo ni bora kwao walionao jua.

Pamoja na ukweli kwamba maisha yetu yanaonekana kujawa na mambo magumu, watu wasumbufu, nyakati ngumu, na matatizo ambayo yako nje ya uwezo wetu; Mhubiri anatuhakikishia kuwa, hayo yana thamani kubwa kuliko yale mazuri tunayotamani kuyapitia maishani mwetu.