Date: 
10-07-2017
Reading: 
Deuteronomy 29:1-9 NIV {Kumbukumbu la Torati 29:1-9}

MONDAY 10 TH JULY 2017  MORNING                                   

Deuteronomy 29:1-9 NIV

Renewal of the Covenant

1 [a]These are the terms of the covenant the Lord commanded Moses to make with the Israelites in Moab, in addition to the covenant he had made with them at Horeb.

Moses summoned all the Israelites and said to them:

Your eyes have seen all that the Lord did in Egypt to Pharaoh, to all his officials and to all his land. With your own eyes you saw those great trials, those signs and great wonders. But to this day the Lord has not given you a mind that understands or eyes that see or ears that hear.Yet the Lord says, “During the forty years that I led you through the wilderness, your clothes did not wear out, nor did the sandals on your feet. You ate no bread and drank no wine or other fermented drink. I did this so that you might know that I am the Lord your God.”

When you reached this place, Sihon king of Heshbon and Og king of Bashan came out to fight against us, but we defeated them. We took their land and gave it as an inheritance to the Reubenites, the Gadites and the half-tribe of Manasseh.

Carefully follow the terms of this covenant, so that you may prosper in everything you do.

Footnotes:

  1. Deuteronomy 29:1 In Hebrew texts 29:1 is numbered 28:69, and 29:2-29 is numbered 29:1-28.                                                 

God was faithful to the Israelites in many ways as is described in this passage. He is faithful to us. God blesses us and provides for us and protects us in many ways. Look out every day for the hand of God in your life. Trust God and obey Him always. This will bring blessing in your life and in the lives of those around you. 

JUMATATU TAREHE 10 JULAI 2017 ASUBUHI  

KUMBUKUMBU YA TORATI  29:1-9      

1 Haya ndiyo maneno ya agano Bwana alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu. 
Musa akawaita Israeli wote akawaambia, Mmeyaona yote Bwana aliyomfanya Farao katika nchi ya Misri mbele ya macho yenu, yeye na watumwa wake wote, na nchi yake yote; 
yale majaribu makuu yaliyoyaona macho yako; hizo ishara, na ile miujiza mikuu; 
lakini Bwana hakuwapa moyo wa kujua, wala macho ya kuona, wala masikio ya kusikia, hata leo hivi. 
Nami miaka arobaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako. 
Hamkula mkate, wala hamkunywa divai, wala kileo; ili mpate kujua kwamba Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu. 
Nanyi mlipokuja mahali hapa, walitutokea kupigana juu yetu Sihoni mfalme wa Heshboni, na Ogu mfalme wa Bashani, tukawapiga; 
tukaitwaa nchi yao, nayo tukawapa Wareubeni, na Wagadi, na nusu ya kabila ya Manase, iwe urithi. 
Shikeni basi maneno ya agano hili myafanye, ili mfanikiwe katika yote mfanyayo. 

Mungu alikuwa mwaminifu kwa Waisraeli na kuwabariki na kuwatunza kwa njia nyingi kama ilivyoelezwa katika somo letu la leo. Mungu pia ni mwaminifu kwetu sisi wakristo tunapomtegemea. Kabidhi kamaisha yako kwa Yesu kila siku na umtii. Ukifanya hivi wewe utabarikiwa na utakuwa Baraka kwa watu wanaokuzunguka.