Date: 
10-10-2019
Reading: 
Daniel 6:18-24

THURSDAY 10TH OCTOBER 2019 MORNING  DANIEL 6:18-24

Daniel 6:18-24 New International Version (NIV)

18 Then the king returned to his palace and spent the night without eating and without any entertainment being brought to him. And he could not sleep.

19 At the first light of dawn, the king got up and hurried to the lions’ den. 20 When he came near the den, he called to Daniel in an anguished voice, “Daniel, servant of the living God, has your God, whom you serve continually, been able to rescue you from the lions?”

21 Daniel answered, “May the king live forever! 22 My God sent his angel, and he shut the mouths of the lions. They have not hurt me, because I was found innocent in his sight. Nor have I ever done any wrong before you, Your Majesty.”

23 The king was overjoyed and gave orders to lift Daniel out of the den. And when Daniel was lifted from the den, no wound was found on him, because he had trusted in his God.

24 At the king’s command, the men who had falsely accused Daniel were brought in and thrown into the lions’ den, along with their wives and children. And before they reached the floor of the den, the lions overpowered them and crushed all their bones.

Daniel was kept perfectly safe, because he believed in his God. Those who boldly and cheerfully trust in God to protect them in the way of duty shall always find him a present help. We must trust in God’s power and faithfulness, not to work a miracle, but commit ourselves to him as a righteous Judge.


ALHAMISI TAREHE 10 MWEZI OKTOBA 2019  ASUBUHI  DANIELI 6:18-24

Danieli 6:18-24

18 Kisha mfalme akaenda nyumbani kwake, akakesha usiku kucha, akafunga; na vinanda havikuletwa mbele yake; na usingizi wake ukampaa.
19 Asubuhi mfalme akaondoka mapema, akaenda kwa haraka mpaka penye lile tundu la simba.
20 Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danielii kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danielii, Ee Danielii, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?
21 Ndipo Danielii akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.
22 Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.
23 Basi mfalme akafurahi sana, akaamuru wamtoe Danielii katika lile tundu. Ndipo Danielii akatolewa katika lile tundu, wala dhara lo lote halikuonekana mwilini mwake, kwa sababu alikuwa anamtumaini Mungu wake.
24 Mfalme akaamuru, nao wakawaleta wale watu waliomshitaki Danielii, wakawatupa katika tundu la simba, wao, na watoto wao, na wake zao; na wale simba wakawashinda wakaivunja mifupa yao vipande vipande, kabla hawajafika chini ya tundu.

Danieli hakupata madhara yoyote, kwa sababu alimwamini Mungu wake. Wale wanaojitoa kwa ujasiri kumtumaini Mungu ili afanyike kinga yao, atawaonekania katika shida zao. Tunapaswa kuamini katika nguvu na uaminifu wa Mungu, siyo kwa ajili ya kupokea muujiza, bali tujitoe kwake kama mwamuzi mwenye haki.