Date: 
05-12-2018
Reading: 
Colossians 1:13-18 (Wakolosai 1:13-18)

WEDNESDAY 5TH DECEMBER  2018 MORNING                            

Colossians 1:13-18 New International Version (NIV)

13 For he has rescued us from the dominion of darkness and brought us into the kingdom of the Son he loves, 14 in whom we have redemption, the forgiveness of sins.

The Supremacy of the Son of God

15 The Son is the image of the invisible God, the firstborn over all creation. 16 For in him all things were created: things in heaven and on earth, visible and invisible, whether thrones or powers or rulers or authorities; all things have been created through him and for him. 17 He is before all things, and in him all things hold together. 18 And he is the head of the body, the church; he is the beginning and the firstborn from among the dead, so that in everything he might have the supremacy.

Jesus Christ was present and active with God the Father in the creation of the universe. He is also our Saviour and the head of the Church.  Let us worship and adore our Lord.

JUMATANO TAREHE 5 DISEMBA 2018 ASUBUHI                   

KOLOSAI 1:13-18

13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake; 
14 ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, msamaha wa dhambi; 
15 naye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. 
16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake. 
17 Naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana katika yeye. 
18 Naye ndiye kichwa cha mwili, yaani, cha kanisa; naye ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, ili kwamba awe mtangulizi katika yote. 

Yesu Kristo, mwana wa Mungu, alikuwepo na alihusika pamoja na Mungu Baba katika uumbaji wa Ulimwengu. Yesu pia ni Mwokozi wetu na Kichwa cha Kanisa. Tumtii na tumwabudu.