Date: 
14-09-2017
Reading: 
Acts 7:22-29 NIV ( Matendo 7:22-29)

THURSDAY 14TH SEPTEMBER 2017 MORNING                        

Acts 7:22-29 New International Version (NIV)

22 Moses was educated in all the wisdom of the Egyptians and was powerful in speech and action.

23 “When Moses was forty years old, he decided to visit his own people, the Israelites. 24 He saw one of them being mistreated by an Egyptian, so he went to his defense and avenged him by killing the Egyptian.25 Moses thought that his own people would realize that God was using him to rescue them, but they did not. 26 The next day Moses came upon two Israelites who were fighting. He tried to reconcile them by saying, ‘Men, you are brothers; why do you want to hurt each other?’

27 “But the man who was mistreating the other pushed Moses aside and said, ‘Who made you ruler and judge over us? 28 Are you thinking of killing me as you killed the Egyptian yesterday?’[a] 29 When Moses heard this, he fled to Midian, where he settled as a foreigner and had two sons.

Footnotes:

  1. Acts 7:28 Exodus 2:14

What Moses did in killing the Egyptian was not right but his intention to stop the oppression of his people was good.  Christ asks us to love and pray for our enemies. We need to stand up for right in all situations and not be afraid. Let us stand up for truth and justice even when the results may be painful for us.

ALHAMISI TAREHE 14 SEPTEMBA 2017 ASUBUHI                   

MATENDO 7:22-29

22 Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo. 
23 Umri wake ulipopata kama miaka arobaini akaazimu moyoni mwake kwenda kuwatazama ndugu zake Waisraeli. 
24 Akamwona mmoja akidhulumiwa, akamtetea, akamlipia kisasi yule aliyekuwa akionewa, akampiga huyo Mmisri. 
25 Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake, lakini hawakufahamu. 
26 Siku ya pili yake akawatokea walipokuwa wakishindana, akataka kuwapatanisha, akisema, Enyi bwana zangu, ninyi ni ndugu. Mbona mnadhulumiana? 
27 Lakini yeye aliyemdhulumu mwenziwe akamsukumia mbali, akisema, Ni nani aliyekuweka wewe kuwa mkuu na mwamuzi juu yetu? 
28 Je! Wataka kuniua mimi kama ulivyomwua yule Mmisri jana? 
29 Musa akakimbia kwa neno hilo, akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Midiani, akazaa wana wawili huko. 

Musa kumuua Mmisri ilikuwa ni kosa. Lakini alikuwa na nia nzuri kumsaidia Mwisraeli mwenzake aliyeteswa. Tunapaswa kutetea wanyonge. Pia Yesu anatuambia tupende maadui zetu. Mungu atusaidie kutetea ukweli na haki hata kama matokeo yake yanatuumiza.