Date: 
22-09-2020
Reading: 
2Chronicles 30:13-20 (2 Nyakati 30:13-20)

TUESDAY 22ND  SEPTEMBER 2020    MORNING                             

2Chronicles 30:13-20 New International Version (NIV)

13 A very large crowd of people assembled in Jerusalem to celebrate the Festival of Unleavened Bread in the second month. 14 They removed the altars in Jerusalem and cleared away the incense altars and threw them into the Kidron Valley.

15 They slaughtered the Passover lamb on the fourteenth day of the second month. The priests and the Levites were ashamed and consecrated themselves and brought burnt offerings to the temple of the Lord. 16 Then they took up their regular positions as prescribed in the Law of Moses the man of God. The priests splashed against the altar the blood handed to them by the Levites. 17 Since many in the crowd had not consecrated themselves, the Levites had to kill the Passover lambs for all those who were not ceremonially clean and could not consecrate their lambs[a] to the Lord. 18 Although most of the many people who came from Ephraim, Manasseh, Issachar and Zebulun had not purified themselves, yet they ate the Passover, contrary to what was written. But Hezekiah prayed for them, saying, “May the Lord, who is good, pardon everyone 19 who sets their heart on seeking God—the Lord, the God of their ancestors—even if they are not clean according to the rules of the sanctuary.” 20 And the Lord heard Hezekiah and healed the people.

What is most needful as we come before God is our broken hearts. God showed his mercy and goodness to those who had prepared their heart to seek Him, though in ignorance they did not eat the Passover according to the commandments. We may not understand doctrine, creed, or rite; but let us be sure to seek God.


JUMANNE TAREHE 22 SEPTEMBER 2020     ASUBUHI               

2 NYAKATI 30:13-20

13 Basi wakakusanyika Yerusalemu watu wengi ili kuifanya sikukuu ya mikate isiyochachwa katika mwezi wa pili, kusanyiko kuu sana.
14 Wakainuka, wakaziondoa madhabahu zilizokuwamo Yerusalemu, nazo madhabahu za kufukizia wakaziondoa, wakazitupa katika kijito Kidroni.
15 Kisha wakaichinja pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili, nao makuhani na Walawi wakatahayarika, wakajitakasa, wakaleta sadaka za kuteketezwa nyumbani mwa Bwana.
16 Wakasimama mahali pao kwa taratibu yao, sawasawa na torati ya Musa, mtu wa Mungu; nao makuhani wakainyunyiza damu, waliyoipokea mikononi mwa Walawi.
17 Kwa maana kulikuwa na wengi katika kusanyiko ambao hawajajitakasa; kwa hiyo Walawi wakamchinjia pasaka, kila mtu asiyekuwa safi, ili kuwatakasa kwa Bwana.
18 Kwani wingi wa watu, naam, wengi wa Efraimu, na wa Manase, na wa Isakari, na wa Zabuloni, hawakujisafisha, lakini wakala pasaka, ila si kama ilivyoandikwa. Naye Hezekia alikuwa amewaombea, akisema, Bwana mwema na amsamehe kila mtu,
19 aukazaye moyo wake kumtafuta Mungu, Bwana, Mungu wa babaze, hata ikiwa si kwa utakaso wa patakatifu.
20 Bwana akamsikia Hezekia, akawaponya watu.

Jambo lililo muhimu zaidi tunapokuja mbele za Mungu ni mioyo iliyopondeka. Mungu alionyesha huruma na wema wake kwa wale wote waliokuwa wameandaa mioyo yao ili kumtafuta, ingawa kwa kutojua kwao, hawakula Pasaka kama ilivyoamriwa. Inawezekana tusijue mafundisho sahihi, ukiri wa imani au taratibu za kanisa; lakini tujihakikishe kuwa tunamtafuta Mungu.