Date: 
08-06-2017
Reading: 
2 Wakorintho 1:3-10 {2Corinthians 1:3-10}

ROHO MTAKATIFU NDIYE MSAADA WETU: NDIYE MFARIJI

2 Wakorintho 1:3-10

Wengi tunamjua Roho Mtakatifu kuwa ni sehemu ya Uungu wa Mungu wetu, yaani moja ya nafsi Tatu za Mungu zinazotimiza Uungu, Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu! Lakini zaidi ya kujiridhisha kumjua hivi, tunahitaji kumjua katika nafasi yake nyingine ya Mfariji! Kuna mambo yake mengi mazuri ya kujifunza kwake! Wewe unajua kuwa Roho Mtakatifu ni;

  • Chanzo au limbuko la nguvu zeta, (Mdo 1:8)?
  • Ni Mwalimu mzuri (Yn 14:26),hata yale tunayosahau hutukumbusha?
  • Hufunua siri na kutujulisha juu ya mambo yajayo? (Yn 16:13)

Japo yote haya ni mazuri, hili la kuwa mfariji (Yn 14:26, Mdo 9:31) linafurahisha na kupendeza sana kwetu wengi! 

Kama umepata kufarijiwa naye, basi nawe utaweza kuwafariji wengine wakiwa katika vipindi vya uchungu na matatizo (2 Wakorintho 1:4); kwani ungependa kila mtu aonje kile ulichopata! Na kama katika maisha yako hujapata kuwa na huzuni,hutaweza kumfariji aliye katika huzuni, kwa kuwa huijui ikoje, wala unatokaje huko. 

Pale tunapopata shida itokanayo na majanga na misiba au fadhaa nyingine yoyote, wengi kikubwa watakachokuambia ni "jipe moyo" au "pole sana, tuko pamoja" na maneno kama hayo. Lakini kwa kuwa nafsi haikuumbwa kubeba uchungu, pekee anayeweza kukupa faraja ya kweli na idumuyo ni Roho Mtakatifu, huduma yake ya faraja ni muhimu katika kuponya majeraha ya ndani. 

Je unapita katika gumu lolote? Una uchungu ndani yako na hakuna awezaye kukufariji? Mgeukie Roho Mtakatifu naye atakupa faraja isiyokwisha katika Jina la Yesu!

HOLY SPIRIT IS OUR HELPER:THE COMFORTER

2 Corinthians 1:3-10

We all know the Holy Spirit to be part of the God Head, that is one of the three persons of God, the Father, the Son and the Holy Spirit. But in addition to all that you also need to know Him the Comforter. There are marvelous things we need to know about the Holy Spirit. Do you know that ;

  • He is the Source of our power (Acts 1:8)
  • He is a Wonderful Teacher (John 14:26)
  • He is a Revealer of secrets and of the future (John 16:13)

As wonderful as all these characteristics are, one characteristic that I find so fascinating is that He is the Comforter (John 14:26). If you have experienced Hima as a Comforter, you will be able to comfort others in distress (2 Corinthians 1:4). If you have not experienced sorrow, you cannot be of much use in comforting the sorrowful.  When we encounter trade goes and sorrowful situations, the best that people can do is to say comforting words like, "take heart", "so sorry ", etc, 

In such situations the ministry of the of the Comforter is needed to heal the hurt deep inside. Are you presently going through a sad situation? Are you so sorrowful that all human attempts at comforting you have failed? The Holy Spirit will reach out and comfort You today, in the name Jesus.