Date: 
29-11-2019
Reading: 
2 Timothy 4:1-8

FRIDAY 29TH NOVEMBER 2019 MORNING                                                     

2 Timothy 4:1-8 New International Version (NIV)

1 In the presence of God and of Christ Jesus, who will judge the living and the dead, and in view of his appearing and his kingdom, I give you this charge: Preach the word; be prepared in season and out of season; correct, rebuke and encourage—with great patience and careful instruction. For the time will come when people will not put up with sound doctrine. Instead, to suit their own desires, they will gather around them a great number of teachers to say what their itching ears want to hear. They will turn their ears away from the truth and turn aside to myths. But you, keep your head in all situations, endure hardship, do the work of an evangelist, discharge all the duties of your ministry.

For I am already being poured out like a drink offering, and the time for my departure is near. I have fought the good fight, I have finished the race, I have kept the faith. Now there is in store for me the crown of righteousness, which the Lord, the righteous Judge, will award to me on that day—and not only to me, but also to all who have longed for his appearing.

We must be aware that God has called Christians to preach in our daily lives; and where necessary, to use words. Every believer must ensure that their daily lives speak more than words; and God’s people grow in grace and truth


IJUMAA TAREHE 29 NOVEMBA 2019  ASUBUHI                                       

2TIMOTHEO 4:1-8

1 Nakuagiza mbele za Mungu, na mbele za Kristo Yesu, atakayewahukumu walio hai na waliokufa; kwa kufunuliwa kwake na kwa ufalme wake;
lihubiri neno, uwe tayari, wakati ukufaao na wakati usiokufaa, karipia, kemea, na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho.
Maana utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima; ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia waalimu makundi makundi, kwa kuwa wana masikio ya utafiti;
nao watajiepusha wasisikie yaliyo kweli, na kuzigeukia hadithi za uongo.
Bali wewe, uwe na kiasi katika mambo yote, vumilia mabaya, fanya kazi ya mhubiri wa Injili, timiliza huduma yako.
Kwa maana, mimi sasa namiminwa, na wakati wa kufariki kwangu umefika.
Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;
baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.

Ni lazima tutambue kuwa Mungu ametuita Wakristo kuhubiri kupitia maisha yetu ya kila siku; na pale itakapobidi, tutumie maneno. Kila Mkristo ahakikishe kuwa, matendo yake ya kila siku yanazungumza zaidi kuliko maneno; na watu wa Mungu wazidi kukua katika neema na kweli.