Date: 
05-06-2019
Reading: 
2 Corinthians 5:1-10 (2 Korintho 5:1-10)

WEDNESDAY 5TH JUNE 2019 MORNING                                        

2 Corinthians 5:1-10 New International Version (NIV)

Awaiting the New Body

1 For we know that if the earthly tent we live in is destroyed, we have a building from God, an eternal house in heaven, not built by human hands. Meanwhile we groan, longing to be clothed instead with our heavenly dwelling, because when we are clothed, we will not be found naked. For while we are in this tent, we groan and are burdened, because we do not wish to be unclothed but to be clothed instead with our heavenly dwelling, so that what is mortal may be swallowed up by life. Now the one who has fashioned us for this very purpose is God, who has given us the Spirit as a deposit, guaranteeing what is to come.

Therefore we are always confident and know that as long as we are at home in the body we are away from the Lord. For we live by faith, not by sight. We are confident, I say, and would prefer to be away from the body and at home with the Lord. So we make it our goal to please him, whether we are at home in the body or away from it. 10 For we must all appear before the judgment seat of Christ, so that each of us may receive what is due us for the things done while in the body, whether good or bad.

The Apostle Paul says that we are longing to go to heaven to be with the Lord. Is this truly our desire or are ambitions just in this life?

Let us remember that our life on earth is like a journey. Let us live to please God and prepare for Eternal Life in heaven with the Lord.


JUMATANO TAREHE 5 JUNI 2019 ASUBUHI                         

2 WAKORINTHO 5:1-10

1 Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. 
Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; 
ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. 
Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima. 
Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho. 
Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. 
(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) 
Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. 
Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. 
10 Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.  

Mtume Paulo anasema kwamba tunatamani kwenda mbinguni kuwa na Mungu wetu. Kweli unatamani kwenda mbinguni au mawazo yako ni hapa duniani tu?

Tukumbuke kwamba maisha hapa duniani ni kama safari tu kuelekea Mbinguni. Ni maandalizi kwa maisha ya baadaye. Tujitahaidi kuishi maisha yanayompendeza Mungu na tujiandae kwa maisha ya Milele na Mungu wetu.