Date: 
01-04-2020
Reading: 
2 Corinthians 4:14-19 (2 Wakorintho 4:14-19)

WEDNESDAY 01ST APRIL 2020  MORNING                                      

2 Corinthians 4:14-19 New International Version (NIV)

 14 For Christ’s love compels us, because we are convinced that one died for all, and therefore all died. 15 And he died for all, that those who live should no longer live for themselves but for him who died for them and was raised again.

16 So from now on we regard no one from a worldly point of view. Though we once regarded Christ in this way, we do so no longer. 17 Therefore, if anyone is in Christ, the new creation has come:[a] The old has gone, the new is here! 18 All this is from God, who reconciled us to himself through Christ and gave us the ministry of reconciliation: 19 that God was reconciling the world to himself in Christ, not counting people’s sins against them. And he has committed to us the message of reconciliation.

Christ died for everyone so that those who believe in Him and accept to change their old ways of life will no longer live for themselves but for Christ, who died and was raised for them. 

And Christ gave us this wonderful message of reconciliation that anyone who belongs to Him has become a new person. The old sinful life is gone; a new life has begun.


JUMATANO TAREHE 01 APRILI 2020  ASUBUHI                   

2 WAKORINTHO 5:14-19

14 Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote;
15 tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao.
16 Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena.
17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
18 Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho;
19 yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.

Kristo alikufa kwa ajili ya wote ili kwamba wale watakaomwamini na kukubali kuziacha njia zao za kale, wasiishi tena kwa matakwa yao bali kwa Kristo, aliyekufa na kufufuka kwa ajili yao.

Na Kristo alitupa ujumbe huu wa matumaini kuwa, yeyote anayempa maisha yake anakuwa mtu mpya. Maisha ya kale ya uovu yanapita; na maisha mapya huanza.