Date: 
15-08-2020
Reading: 
2 Chronicles 28:8-10

SATURDAY 15TH AUGUST 2020 MORNING                                                 

2 Chronicles 28:8-10 New International Version (NIV)

The men of Israel took captive from their fellow Israelites who were from Judah two hundred thousand wives, sons and daughters. They also took a great deal of plunder, which they carried back to Samaria.

But a prophet of the Lord named Oded was there, and he went out to meet the army when it returned to Samaria. He said to them, “Because the Lord, the God of your ancestors, was angry with Judah, he gave them into your hand. But you have slaughtered them in a rage that reaches to heaven. 10 And now you intend to make the men and women of Judah and Jerusalem your slaves. But aren’t you also guilty of sins against the Lord your God?

Repentance always means acknowledging your own sin, not comparing yourself with others who may be more sinful. As Christians, we have a choice; we forsake God to go after sin or we forsake sin to go after God.


JUMAMOSI TAREHE 15 AGOSTI 2020 ASUBUHI                                           

2 NYAKATI 28:8-10

Wana wa Israeli wakachukua wa ndugu zao wafungwa mia mbili elfu, wanawake, na wana, na binti, pia wakachukua kwao nyara nyingi, wakazileta nyara Samaria.
Lakini kulikuwako huko nabii wa Bwana, jina lake aliitwa Odedi; akatoka kuwalaki jeshi waliokuja Samaria, akawaambia, Angalieni, kwa kuwa Bwana, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, yeye amewatia mikononi mwenu, nanyi mmewaua kwa ghadhabu iliyofikia mbinguni.
10 Na sasa mwanuia kuwatawala wana wa Yuda na Yerusalemu, wawe kwenu watumwa na wajakazi; lakini ninyi nanyi je! Hamna hatia zenu wenyewe juu ya Bwana, Mungu wenu?

Toba ya kweli ni kukubali makosa yako, na siyo kujilinganisha na wengine ambao wanaweza kuwa na dhambi zaidi yako. Sisi kama Wakristo, tunao uchaguzi; ama kumwacha Mungu na kufuata dhambi au kuziacha dhambi na kumfuata Mungu.