Date: 
26-08-2020
Reading: 
1Thessalonians 2:1-8

WEDNESDAY 26TH AUGUST 2020  MORNING                                       

1Thessalonians 2:1-8  New International Version (NIV)

You know, brothers and sisters, that our visit to you was not without results. We had previously suffered and been treated outrageously in Philippi, as you know, but with the help of our God we dared to tell you his gospel in the face of strong opposition. For the appeal we make does not spring from error or impure motives, nor are we trying to trick you. On the contrary, we speak as those approved by God to be entrusted with the gospel. We are not trying to please people but God, who tests our hearts. You know we never used flattery, nor did we put on a mask to cover up greed—God is our witness. We were not looking for praise from people, not from you or anyone else, even though as apostles of Christ we could have asserted our authority. Instead, we were like young children[a] among you.

Just as a nursing mother cares for her children, so we cared for you. Because we loved you so much, we were delighted to share with you not only the gospel of God but our lives as well. 

As Christians, we are all community builders; and we are called for each one of us to interact with one another in our present Christian community with bold speech, personal integrity, and strengthening each other with God’s word.


JUMATANO TAREHE 26 AGOSTI 2020  ASUBUHI                               

1 WATHESALONIKE 2:1-8

1 Maana ninyi wenyewe, ndugu, mwakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure;
2 lakini tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filipi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.
3 Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila;
4 bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.
5 Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.
6 Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa Kristo;
7 bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.
8 Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.

Sisi Wakristo ni jamii ya wajenzi; na tunaitwa kila mmoja wetu kuhusiana na wengine katika jamii tunayoishi kwa kuzungumza kwa ujasiri, kuishi kwa uaminifu na kuimarishana kwa neno la Mungu.