Date: 
09-03-2022
Reading: 
1 Wakorintho 10:12-13

Hii ni Kwaresma 

Jumatano asubuhi tarehe 09.03.2022

1 Wakorintho 10:12-13

12 Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.

13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

Tukimtegemea Bwana Tutashinda majaribu;

Mtume Paulo anawaandikia waKorintho akiwaambia kuwa anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Mtume Paulo hapa anatoa usia kwa Kanisa kusimama imara katika imani, ili tusije kumuasi Mungu wetu.

Paulo anaonesha kuwa penye majaribu, siku zote Mungu yuko na watu wake. Hawezi kuruhusu wajaribiwe zaidi ya walivyo, na huwasaidia kushinda majaribu. Hapa tunakumbushwa kuwa ni Mungu pekee atuwezeshaye kushinda majaribu katika maisha yetu.

Tuishikilie imani yetu kwa kumtegemea Mungu ili atuepushe na majaribu, tunapoiendea njia ya uzima wa milele.

Nakutakia Jumatano njema.

Hii ni Kwaresma