Date: 
30-09-2022
Reading: 
1 Samweli 16:1-10

Ijumaa asubuhi tarehe 30.09.2022

1 Samweli 16:1-10

1 Bwana akamwambia Samweli, Hata lini utamlilia Sauli, ikiwa mimi nimemkataa asiwamiliki Israeli? Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.

2 Samweli akasema, Nawezaje kwenda? Sauli akipata habari, ataniua. Basi Bwana akasema, Chukua ndama pamoja nawe, ukaseme, Nimekuja ili kumtolea Bwana dhabihu.

3 Ukamwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha utakayotenda; nawe utamtia mafuta yule nitakayemtaja kwako.

4 Samweli akafanya hayo aliyosema Bwana, akaenda Bethlehemu. Wakaja wazee wa mji kumlaki, wakitetemeka, nao wakasema, Je! Umekuja kwa amani?

5 Naye akasema, Naam, kwa amani; nimekuja kumtolea Bwana dhabihu; jitakaseni; njoni pamoja nami kwenye dhabihu. Akawatakasa Yese na wanawe, akawaita kwenye dhabihu.

6 Ikawa walipokuja, alimtazama Eliabu, akasema, Yakini masihi wa BWANA yupo hapa mbele zake.

7 Lakini Bwana akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo.

8 Ndipo Yese akamwita Abinadabu, akampitisha mbele ya Samweli. Naye akasema, Bwana hakumchagua huyu.

9 Ndipo Yese akampitisha Shama. Naye akasema, wala Bwana hakumchagua huyu.

10 Yese akawapitisha wanawe saba mbele ya Samweli. Samweli akamwambia Yese, Bwana hakuwachagua hawa.

Uchaguzi wa busara;

Samweli alitumwa kwenda kwa Yese ampake Mfalme mafuta. Yese akawaleta watoto wote, hakuna aliyemchagua Bwana. Bwana alimwambia Samweli asiangalie uso wala urefu, maana yeye hutazama moyo. Ndipo baadaye akaletwa Daudi, akapakwa mafuta kuwa mfalme.

Samweli alimchagua mfalme kwa kuelekezwa na Bwana. Kumbe tukitaka kufanya vizuri, tuongozwe na Bwana. Tunaalikwa kufanya uchaguzi wa kuongozwa na Bwana katika kazi zetu, ili tufanye uchaguzi sahihi ulio wa busara kuelekea uzima wa milele.

Ijumaa njema.