Date: 
01-05-2020
Reading: 
1 Samuel 17:31-37

FRIDAY 1ST MAY 2020   MORNING                                                             

1 Samuel 17:31-37 New International Version (NIV)

31 What David said was overheard and reported to Saul, and Saul sent for him.

32 David said to Saul, “Let no one lose heart on account of this Philistine; your servant will go and fight him.”

33 Saul replied, “You are not able to go out against this Philistine and fight him; you are only a young man, and he has been a warrior from his youth.”

34 But David said to Saul, “Your servant has been keeping his father’s sheep. When a lion or a bear came and carried off a sheep from the flock, 35 I went after it, struck it and rescued the sheep from its mouth. When it turned on me, I seized it by its hair, struck it and killed it. 36 Your servant has killed both the lion and the bear; this uncircumcised Philistine will be like one of them, because he has defied the armies of the living God. 37 The Lord who rescued me from the paw of the lion and the paw of the bear will rescue me from the hand of this Philistine.”

Saul said to David, “Go, and the Lord be with you.”

This story does not prove the courage and skill of David but the protection of God to those who put their trust in Him.

It can happen to us too that we find ourselves capable of taking on challenges that we believed were beyond our ability.

Let us remember the words of Paul, “I can do everything in Him who gives me strength” and “When I am weak, then I am strong” (Philippians 4:13;     2 Cor. 12:10b).


IJUMAA TAREHE 1 MEI 2020  ASUBUHI                                                       

1SAMWEL 17:31-37

31 Na maneno hayo aliyosema Daudi yaliposikiwa, watu wakamweleza Sauli; naye akatuma mtu kwenda kumwita.
32 Daudi akamwambia Sauli, Asizimie moyo mtu ye yote kwa ajili ya huyu; mimi mtumishi wako nitakwenda kupigana na Mfilisti huyu.
33 Sauli akamwambia Daudi, Huwezi wewe kumwendea Mfilisti huyu upigane naye; maana wewe u kijana tu; na huyu ni mtu wa vita tangu ujana wake.
34 Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi,
35 mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua.
36 Mtumishi wako alimwua simba na dubu pia; na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amewatukana majeshi ya Mungu aliye hai.
37 Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe.

Habari hii haishuhudii ujasiri na mbinu alizokuwa nazo Daudi, bali inadhihirisha ulinzi wa Mungu kwa wale wanaoweka tumaini lao kwake.

Hali hii inaweza kutokea kwetu pia, kwamba tunajikuta tukizishinda changamoto ambazo tuliamini ziko juu ya uwezo wetu.

Tukumbuke maneno ya Mtume Paulo, “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu” na “Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.(Wafilipi 4:13;     2 Kor. 12:10b).