Date: 
06-10-2017
Reading: 
1 Samuel 1:21-25 NIV

FRIDAY 6th OCTOBER 2017 MORNING                          

1 Samuel 1:21-25  New International Version (NIV)

Hannah Dedicates Samuel

21 When her husband Elkanah went up with all his family to offer the annual sacrifice to the Lord and to fulfill his vow, 22 Hannah did not go. She said to her husband, “After the boy is weaned, I will take him and present him before the Lord, and he will live there always.”23 “Do what seems best to you,” her husband Elkanah told her. “Stay here until you have weaned him; only may the Lord make good his word.” So the woman stayed at home and nursed her son until she had weaned him. 24 After he was weaned, she took the boy with her, young as he was, along with a three-year-old bull, an ephah of flour and a skin of wine, and brought him to the house of the Lord at Shiloh. 25 When the bull had been sacrificed, they brought the boy to Eli,

Message:

Hannah took her son to Shiloh, where she dedicated him to God for life. This means that, parents and guardians have to lend their children to God as long as they live. It is very important for these children to continue to be God’s servants. Let us not stop them from experiencing God’s love in their whole life; and this is the right way of showing love to our children. 

IJUMAA TAREHE 6 OKTOBA 2017 ASUBUHI                         

1 Sam 1:21-25

 

Kuzaliwa na Kuwekwa Wakfu kwa Samweli

21 Kisha yule mtu, Elkana, na watu wote wa nyumbani mwake, wakakwea kwenda kumtolea Bwana dhabihu ya mwaka, na nadhiri yake. 
22 Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa maziwa, hapo ndipo nitakapomleta, ili ahudhurie mbele za Bwana, akae huko daima. 
23 Elkana, mumewe, akamwambia, Haya, fanya uonavyo vema; ngoja hata utakapomwachisha maziwa; Bwana na alithibitishe neno lake tu. Basi yule mwanamke akangoja, akamnyonyesha mtoto wake, hata akamwachisha maziwa. 
24 Naye alipokuwa amekwisha kumwachisha maziwa, akamchukua pamoja naye, na ng'ombe watatu, na efa moja ya unga,na chupa ya divai,akamleta nyumbani kwa BWANA,huko Shilo ;na Yule mtoto alikuwa mtoto mdogo. 
25 Nao wakamchinja huyo ng'ombe, wakamleta mtoto kwa Eli. 

Ujumbe:

Hana alimpeleka mtoto wake kule Shilo ili aweze kumweka wakfu mbele za Mungu. Maana yake ni kwamba, ni wajibu wa wazazi na walezi kuwaachilia watoto wao ili Mungu awatumie wakati wa uhai wao wote. Ni muhimu kwa hawa watoto kuendelea kutumika mbele za Mungu. Tuwaruhusu kukutana na upendo wa Mungu katika maisha yao; na hii ndiyo njia sahihi ya kuonyesha upendo kwa watoto wetu.