Date: 
01-08-2018
Reading: 
1 Corinthians 1:26-31 (1Wakorintho 1:26-31)

WEDNESDAY 1ST AUGUST 2018 MORNING                

1 Corinthians 1:26-31 New International Version (NIV)

26 Brothers and sisters, think of what you were when you were called. Not many of you were wise by human standards; not many were influential; not many were of noble birth. 27 But God chose the foolish things of the world to shame the wise; God chose the weak things of the world to shame the strong. 28 God chose the lowly things of this world and the despised things—and the things that are not—to nullify the things that are, 29 so that no one may boast before him. 30 It is because of him that you are in Christ Jesus, who has become for us wisdom from God—that is, our righteousness, holiness and redemption. 31 Therefore, as it is written: “Let the one who boasts boast in the Lord.”[a]

Footnotes:

  1. 1 Corinthians 1:31 Jer. 9:24

We need the power of the Holy Spirit to enable us to understand God. God can work through our minds when they are sanctified and committed to Him. However sometimes people who are very learned in worldly knowledge reject God. Their human understanding cannot fathom Him. They may only believe what can be measured scientifically.

Let us ask God to enlighten our minds and us into all His truth. God is the source of all truth.

JUMATANO TAREHE 1 AGOSTI 2018 ASUBUHI                    

1 KORINTHO 1:26-31

26 Maana, ndugu zangu, angalieni mwito wenu, ya kwamba si wengi wenye hekima ya mwilini, si wengi wenye nguvu, si wengi wenye cheo walioitwa; 
27 bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu; 
28 tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko; 
29 mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu. 
30 Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi; 
31 kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.

Tunahitaji nguvu ya Roho Mtakatifu ili tumwelewe Mungu. Mungu anaweza kutumia akili zetu kama tunakubali kuongozwa na Roho Mtakatifu. Lakini kuna watu wenye elimu sana, hasa ya kisayansi, ambao hawaamini Mungu na hawaamini chochote ambacho hakipimiki na sayansi.

Tuelewe akili ya binadamu haiwezi kumpima Mungu.

Tumwombe Mungu atuelimishe na atuongoze. Mungu ni chanzo cha kweli yote.