Date: 
20-10-2021
Reading: 
Wagalatia 6:1-5 (Galatians)

JUMATANO TAREHE 20 OKTOBA 2021, ASUBUHI.

Wagalatia 6:1-5

1 Ndugu zangu, mtu akighafilika katika kosa lo lote, ninyi mlio wa Roho mrejezeni upya mtu kama huyo kwa roho ya upole, ukijiangalia nafsi yako usije ukajaribiwa wewe mwenyewe.

2 Mchukuliane mizigo na kuitimiza hivyo sheria ya Kristo.

3 Maana mtu akijiona kuwa ni kitu, naye si kitu, ajidanganya nafsi yake.

4 Lakini kila mtu na aipime kazi yake mwenyewe, ndipo atakapokuwa na sababu ya kujisifu ndani ya nafsi yake tu, wala si kwa mwenzake.

5 Maana kila mtu atalichukua furushi lake mwenyewe.

Njia ya ufalme wa Mungu;

Asubuhi hii tunasoma habari ya Mtume Paulo akiwaandikia Wagalatia juu ya kuchukuliana mizigo. Anawaasa kumrejesha anayepotea kwa upole. Paulo anaonesha hakuna haja ya kujisifu, la muhimu ni kumfuata Yesu tukiwasaidia wengine kubaki katika njia sahihi.

Ujumbe tunaopewa ni kuhakikisha sisi wenyewe kila mmoja kwa nafasi yake anatimiza utume wa kuhubiri ijili ya Yesu Kristo, ili asiwepo yeyote wa kuukosa ufalme wa Mungu. Je, umetimiza wajibu wako katika hilo?

Siku njema.


WEDNESDAY 20TH OCTOBER 2021, MORNING.

Galatians 6:1-5

Doing Good to All

1 Brothers and sisters, if someone is caught in a sin, you who live by the Spirit should restore that person gently. But watch yourselves, or you also may be tempted. Carry each other’s burdens, and in this way you will fulfil the law of Christ. If anyone thinks they are something when they are not, they deceive themselves. Each one should test their own actions. Then they can take pride in themselves alone, without comparing themselves to someone else, for each one should carry their own load.

Read full chapter

The way to the kingdom of God;

This morning we read the story of the Apostle Paul writing to the Galatians about carrying burdens for one another. He urges them to restore the lost ones’ gently. Paul shows there is no need to brag, the important thing is to follow Jesus while helping others stay on the right path.

The message we are given is to make sure that each of us in our own place fulfils the mission of preaching the gospel of Christ, so that no one will miss the kingdom of God. Have you fulfilled your role in that?

Good day.